Elections 2010 Dr. Slaa lau angejua...


Ndiyo bwana. Ni kweli hasa. Tatizo mara nyingi mtu ukimbana kwenye sehemu zote anashindwa kuwa kimya na kusema chochote. Hiyo ndiyo shida ya watu wachache.
 
Hukuhitaji kuniita Kilaza wakati umerudia yale yote niliyoongea mimi hapo juu. Huu uliosema ndiyo ukweli na utabakia hivyo hivyo kama pia nilivyosema mimi hapo juu.
BW KANYAFU INABIDI TUMWAMBIE Jamii Forum kama ni matusi na masuhabiki wa chadema wamezidi hawa si URAIS tu hata JK walimtukania MAMA YAKE mbona ZITTO na MBOWE katika wapiga kura wa MAJIMBOyao wamenyamaza
JF sisi tunaotumia huu mtandao hatufiki hata 1000 ya nini kuukanana? MIMI SITAKI UPINZANI MAANA LEO CHADEMA KESHO CUF CCM HAMTAITOA kwa matusi
SLAA KAINGIZWA MKENGE HAA TURUDIE CEMENT YA 5000 CHADEMA ACHENI MATUSI
kama mnabisha JF achambue michango yote na awa-block
NCHI HAENDI KWA JAZBA RAIS KESHAAPISHWA
 

Ukwaju, unachosema ni kweli. Mtu wa kawaida akikosa cha kujibu huwa anatukana hasa iwapo suala linamuhusu, badala ya kutafuta suluhisho au kutafakari kitakachofuata. Wenye busara wote huwa wanabakia kimya. Ukweli unabakia pale pale kama thread inavyotanabahisha.
 
Msemakweli n0.2 hizo Data hazifai kwani katika za Msemakweli colum ya 3 inasema Voters to Vote maana yake (wanaotarajiwa kupiga kura) pia hakuna kura zilizoharibika na hakuna kura za visiwani halafu jumla ya waliojiandikisha ni 20.445.725 lakini si kweli wapiga kura ni 13.289.721.25 hakuna mu robo 0.25 bali waliopiga kura ni 8.000.00077
 
Kanyafu Nkanwa,

..I beg to differ.

..sasa kama unasema Chadema wamemtosa Slaa, what can you say about CUF and Lipumba?

..naamini kitendo cha Dr.Slaa kugombea Uraisi kumeijenga Chadema kuliko ambavyo asingegombea.

..msisimko aliouleta SLAA ktk kampeni za uchaguzi umewezesha CHADEMA kupata WABUNGE na WAPENZI wengi zaidi.

..Dr.Slaa gave CCM a run for their money. sote tumeona desperate moves za CCM kama msg za kichochezi, kampeni chafu za kashfa na vitisho[wapinzani wanataka kutumia maiti kupata uongozi] alizolazimika kufanya JK.

..Uchaguzi mkuu ungedorora kwelikweli kama Slaa asingem-challenge JK.

..moving forward, ni rahisi zaidi kwa Chadema kujenga mtandao wa wanachama vijijini tayari kwa uchaguzi wa 2015. mazingira yangekuwa magumu zaidi kama Chadema wasingeshiriki ktk kinyanganyiro cha Uraisi.

..Dr.Slaa amekuwa mpambanaji Bungeni and we know he is good at that. sasa hivi tungependa kuona jinsi gani anachukua challenge mpya ya kukieneza chama vijijini kwa wapiga kura. inatia moyo kwamba Chadema sasa hivi itakuwa na katibu mkuu ambaye hana majukumu ya ubunge, bali ya kujenga na kueneza chama.
 
Kubalini tu mzee slaa this time ameingizwa mjini aisee na wajanja wenzake wengine wa CHADEMA

Kama ni ushabiki tu labda, lakini kusema Slaa ameingizwa mjini ni ujinga (ignorance) wa hali ya juu kabisa. Hakuna alichopungukiwa kwa kazi ya kipekee na ya heshima aliyofanya. Sina haja ya kuelezea alichofanikisha katika uchaguzi huu. Kama ni kushindwa basi ni sisi Watanzania ndio tumeshindwa; ndio tutakaoendelea kupigika na mfumo wa ufisadi unaoushangilia. Mnashangaza sana mnaoleta mada ya aina hii.
 

Watu wengine bwana wanashangaza mno! Hata wanatia 'kichechefu' kusoma maandiko yao.
 
Jamani kwa nini tunapenda mambo ya ushabiki zaidi ya kuliko ukweli na uzalendo wa Taifa hili.
ni na kwenye nchi hii na hata nje ya nchi asiyejua kuwa Chadema kimeshinda kwa kiwango kikubwa na hata ccm. Wenyewe Wanalijua hilo lakini hataki kukubali ndani ya JF. Patakuwa mahali pa heshima sana kama tutakuwa wawazi na kuchambua mambo muhimu na mustakabali wa Taifa hili tuheshimiane Kidemokrasia na sio ushabiki na udaku wa mitaani tu kumbukeni JF. Inajulikana kama THE HOME OF GREAT THINKERS
 

na wewe utakumbukwa na huyo mchaga wako?
 
mawazo gani bwanamzee. ujue kuingia kwa Dr Slaa hakukuwa na maana ya kushinda urais pekee bali kuleta hamasa kwenye kambi ya upinzani. faida za kuingia kwa Dr Slaa zimeonekana wazi. Upinzani umeimarika sana
 
Hey guys do not get worried wakati wote all precautions have been taken into account. Hakuna haja ya jazba na tusiwe pessimistic all the time. AMINi USIAMINI CHADEMA HAS THE TRUST OF WANANCHI NA 2015 NI MWAKA WETU hata JK analijua hilo sasa.
 
Mimi naona kushindwa kwa DR Slaa siyo tatizo kwani nachoamini ni kuwa demecrasia ya kweli huchukua muda mrefu sana kupatikana na uamuzi wa Dr Slaa kugombea ni mojawapo ya hatua katika kuelekea kwenye democrasia ya kweli.Watu wanatakiwa waendelee kupambana na mfumo mbovu wakiwa ndani ya mfumo!siyo wakiwa nje ya mfumo!
 
Kwa hiyo kaka ushauri wako nini mbona sijakuelewa 1. kwamba Watanzania tuendele kuabudu ccm 2.CCM ni mungu wa siasa Tz ambae hawezi ng'oka au 3. Tuamini katika unafiki na uongo? au ujumbe wako hasa nini kwa Watanzania ukiwa Mzalendo uliochoshwa na ubadhilifu wa mali za uma na ufisadi wa ccm :A S angry::A S angry::A S angry::A S angry::nono::nono::nono::doh: :doh:
 

unajua maana halisi ya punje ya ngano wewe? A grain of wheat. Ilikuwa pia si lazima WIS awe rais kwani urais inaweza pia kuwa si hoja sana. Kawezesha nchi kujua ukweli kuhusu siasa za maji taka zinazoendeshwa na ccm. KAwezesha chama kupata wabunge wachapa kazi mno. Bungeni si mahala pekee mtu anaweza kuleta mabadiliko. Kuna wanaharakai wengi wanaleta mabadiliko na hawapo bungeni.

Slaa kazi kubwa aliyo nayo ni kuimarisha chama tangu ngazi ya vitongoji nchi nzima. jukumu ambalo asingeweza kulifanya akiwa mbunge. Tunamheshimu WIS kwa mchango wake na uthubutu wake wa kugombea nafasi hiyo nchini. Kazi ya chama atakayoifanya kwa sasa ni msingi imara wa uchaguzi wa 2015. Cha msingi kuna vijana wa kutosha bungeni kuendeleza mapambano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…