Elections 2010 Dr Slaa ndani ya Bukoba

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
7,904
Reaction score
1,064
Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Dr Willibrod Peter Slaa yupo leo Bukoba. Amekuwa na mkutano maeneo ya Kibengwe Bukoba vijijini na anategemea kuwa Kanyigo baadaye.

Sasa hivi anategemewa muda mfupi ujao atakuwa katika kata ya Ijuganyundo katika Manispaa ya Bukoba. Kisha atahutubia katika viwanja maarufu hapa mjini kama Uhuru Platform. Watu ni wengi sana walio katika maandalizi ya kumpokea na kumsikiliza. Naona bendera kila mahali.

Nimepata habari kwamba kule Karagwe jana Dr alipokelewa na umati ambao haujapata kuonekana na kwa wale wakazi wa Karagwe inasemekana watu walijipanga njiani toka Kayanga hadi Nyaishozi ili kumlaki mwaka huu namshauri Kikwete aondoke kwa amani ikulu.

Habari zaidi na picha baadae wakuu wangu. Ngoja niwahi mkutano!

People's Poweeeeeeeeeeer!

UPDATES - PICHA:


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake, katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Uhuru.



Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akiwapungia mkono wakazi wa mji wa Bukoba katika msafara kuelekea katika Uwanja wa Uhuru mjini mjini Bukoba ambako alifanya mkutano wa kampeni (Picha: Joseph Senga)
 
...... peoples>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> power!!!!!!!!!!


kazi iko haijawahi............... yetu macho. Mwendo mdundo.
 
Tunasubiri habari zaidi toka mkutanoni..
 
Tuletee picture maana kama kuna watu wengi TBC hawataonyesha ukweli...
 
asante sana mchukia ufisadi kwa update, ila usisahau HIZO PICHA ZA RAIS WA TZ
 

May God bless you for this poignant thread
 
Karibu sana shujaa wetu mjini Bukoba! Wananchi wanakiu na njaa wanahitaji uwape kile roho zao zinapenda.

USISAHAU PICHA!
 
Dr Slaa for our unity, diginity and hope. This is the new hope for our country and no one else. We want to be the first country to fight against frauds, in Africa. CCM stop dreaming of descriminating the people's powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr.
 
Si hapo BK Mjini yupo Mbunge Lwakatare kwa tiketi ya Chadema bt nashangaa makeke yake hayasikiki kabisa
 


Go go Our President
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…