Mkutano wa kihistoria. Pale Uhuru platform pamoja na barabara zote nne zinazozunguka uwanja zilijaa watu. wasillizaji wakubwa walikuwa maaskari polisi waliovalia kininja waliokuwa hata hawataki mtu akohoe.(Baadaye niligundua hawakutaka walikose hata neno moja analosema
Slaa). Dr alimwaga sera akieleza maadui 3 aliowaacha mwl Nyerere hawakuthibitiwa sasa wamejaa mtoto jeuri aitwaye ufisadi sasa si watatu tena bali wanne. Akaeleza kumuenzi mwl ni kuendeleza fikra na matendo aliyoyaanzisha. Suala la utaifa na maandalizi ya vijana wa kitanzania yanapaswa kugharamiwa kwa gharama yoyote. Alieleza jinsi Nyerere alivyowapeleka wahaya kusomea Mtwara na Wanyakyusa akawaleta Ngara. Wakati ule hakuna aliyemwelewa na hasa alipotaifisha mashule na kuitwika serkali mzigo wa kuyaendesha. Kumbe alichokuwa anapambana nacho ni kujenga utaifa. Wachaga wakafanya urafiki na wamakonde na kuoa huko huo ukawa mwisho wa uhasama na vita ya makabila. Isitoshe aliwapeleka vijana wote wa kitanzania jkt wakapikwa na kufundishwa uzalendo kwa nchi yao. Leo sisiem wanapeleka vijana kwenye makambi ya green guards ili wajifunze kumwaga damu ya watanzania wenzao badala ya kulinda usalama wa nchi yao. Akasema ndiyo maana serkali ya Chadema inaamua kubeba mzigo mkubwa sana wa kutoa elimu itakayorejesha utaifa kwa kuondoa matabaka ili wote wasome. Amesema wengi wanahoji atatoa wapi fedha lakini anajua kuwa vx wanazotembelea mawaziri wa jk zimebeba gharama ya shule nzima ya sekondari -200mil au dispensari 4. Yeye amekubali kula mihogo ikulu na kutembelea Landcruiser mkonga ili akomboe hela inayotumiwa kwa kuongeza starehe ikulu kusomesha watoto wa kitanzania. Huku akishangiliwa na kukatishwa mara kadhaa na wazee waliotaka kurudisha kadi za ccm alionyesha kuwa kujenga tu zahanati kila kijiji haitoshi kama watu wanaishi katika mazingira hatarishi. Miaka 49 ya uhuru watanzania wanaishi katika nyumba za kuchimba chini ya ardhi, ziliparatwa kwa tope huku vumbi likitimka na kuathiri afya zao. Hata ungejenga zahanati ngapi afya haiwezi kuboreka wakati watu wanaishi katika viroboto na vumbi. Ndiyo maana serkali ya chadema katika kuboresha maisha ya watanzania wa kawaida ili mwl anayepata 160000 ajenge nyumba na askari anayelipwa 200000 ajenge nyumba itaondoa kodi ya serkali katika vifaa vya ujenzi kama simenti na bati. Dr awali alikuwa ameeleza ubaya na madhara ya rushwa na ufisadi na jinsi Chadema imekuwa ikipambana nayo kurudiha tunu za nchi yetu. Amesema Jk anawakumbatia mafisadi wote na hana utashi wala ubavu wowote wa kuwakemea. Rostam Aziz mmiliki wa Kagoda, Andrew Chenge na vituko vya rada, Basil Mramba, ni Chadema tu iliyowahi kujitokeza kupambana na ufisadi tangu Richmond, benki kuu, Rada nk Dr alikazia kuwa hata zile fedha za kusaidia madhara ya mtikisiko wa kiuchumi ambazo wakulima waliadhirika kwa kukosa bei nzuri ya mazao na makampuni yanayonunua mazao yalipata hasara kwa kukosa soko zuri zimeishia mifukoni mwa maswahiba wa kikwete. Amewaomba usalama wa taifa wasidhubutu kujiigiza katika kuchakachua kura kwani watanzania wamekwisha amua wanachokitaka. Hawahitaji kusemewa na Redet wala Synovet maana wao wana midomo yao. Ndipo akauliza eti wangapi watampa Dr Slaa kura tar 31 uwanja mzima ukanyoosha mikono akasema hebu usalama wa taifa chukueni rekodi hiyo. wanagapi watampa jk wote wakashusha mikono. Mwishoni alitoa tamko la chama chake kuwa Chadema haitaki kuingia ikulu kwa kumwaga damu ya mtu. Je tutawaongoza kina nani ikiwa watu tayari wamekufa? Alidai Chadema ni chama cha amani na hawataki damu ya mtu imwagike. Badala yake akamwonya jk kuwazuia green guards waliosambazwa nchi nzima kufanya fujo kwa vyama tofauti na ccm. kama kila chama kikiweka vijana wake kama ccm wanavyoffanya ili kuwadhibiti green guard patakuwa hapakaliki tena. Na hiyo fujo itakuwa imeanzishwa na ccm. Pia aliwaambia usalama wa taifa wasijaribu kabisa kuchakachua kura maana mipango yao amekwisha inasa. Amesema ataileza wakati ukifika. Saa 12 akafunga mkutano na watu kwa furaha wakaagana naye na wengine kuchangia gharama za mafuta ya helikopta. Wazee wawili waliokaa kando ya msikiti wa uswahilini wakasikika wakisema uwanja huu umekuwa na mikutano mingi lakini huu ni kwanza wa aina yake. Watu wengi, maneno mazuri, asiyempa kura baba huyu ana lake jambo!!!!!!!