Dr Slaa AKUMBUKE kutamka wazi kuwa anawapenda wana CCM na aendee kuziomba kura zao kama alivyofanya mwanzoni. Hata wana ccm wenyewe wameishamchoka Kikwete. Asisitize kuwa wana CCM wengi wana mapenzi mema na nchi yao, na hata yeye anawapenda. Isipokuwa CCM imekuwa ya mafisadi wachache,ndio wanaofaidi. Wana ccm wengi waliobaki, pamoja na ushabiki hawana wanachokifaidi ndani ya Chama chao. Asisitize kuwa yeye ndiye mkombozi wa wote na hasa wana CCM!
Kauli kama hii yaweza kuvuta hisia na kubadili mawazo ya watu kwa haraka sana. Dr Slaa ukumbuke ulivyomsema vizuri Mwakyembe ulikuwa kivutio, ukabadili hisia za watu na kusababisha wana ccm wote wakukubali. Dr Slaa sasa wasifie wana CCM. Toa kauli nzuri kwamba wewe ni mkombozi wa Wana ccm. Adui mkubwa wa Chadema ni mafisadi na sio wana CCM. Tafadhali Dr Slaa usisitize jambo hili. Maana watu wasio na uelewa wanakatana mapanga wakidhani wewe utakuwa rais wa wana CHADEMA na hivi kuwatelekeza wao.