Dr. Slaa: Serikali tatu si pendekezo la CHADEMA

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
5,597
Reaction score
1,013
Akizungumza katika kipindi cha hotmix kinachorushwa na EATV, DK SLAA AMESEMA SUALA LA SERIKALI TATU SI LA CHADEMA BALI NI LA TUME YA WARIOBA. Amesema kuwa wanaotaka serikali mbili ni sawa na kuvunja msingi (foundation) iliyowekwa na tume iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba.
 
Slaa nitaruhusu gongo nikishinda

Serikali tatu ni kama gongo tuu
 
huoni aibu unapotosha
Kazungumza kudumisha Muungano.

Hakutamka muundo wa Muungano kuwa serikali 2 au 3
 
Yote yazungmzwe na kujadiliwa lakini tunahitaji maoni ya wananchi yapewe kipaumbele.

Tumependekeza kupitia tume kuwa ni serikali 3.

Swala la muungano ni la kujadili,na jibu lake ni uwepo au usiwepo.

Binafsi sioni faida yake...uvunjwe ili kila pande ijue inakosa vitu gani pasipo muungano.
 
kumbe ni tume ya warioba,tulidhani ni mawazo ya watanzania tena walio wengi.serikali 3 tupa kule
 
yap yap,lamsingi ni wananchi waamue,hatuwezi kufanyia kazi mawazo ya watu wachache tu.cku zote wengi wape..
 
Slaa ni mnafiki tu! wamezunguka nchi nzima sio kutoa elimu ya katiba kwa wananchi bali ni kuwashawishi wananchi wafate itikadi ya chama chao leo asitudanganye kuwa wazo la serikali tatu sio la chadema huo ni uongo
 
Ah ,huyo Slaa nae kama Dallai Lama hajulikani kama ni China au Tibet.
 
Hilo ndilo tatizo la wanasiasa wengi wa nchi yetu wapo kama bendera ufuata upepo,nilimsikiliza mwanzo mwisho nilicho kiona kwake ni kanyaga twende,ila ngoja tuone maana mwisho wasiku kauli ya mwisho ipo kwetu kwanjia yakura,TUWASUBIRI,
 

Unanikosha! Ukiondoa Marekani, nchi nyingine zote zimeshindwa kudumisha Muungano kwa kuwa MIUNGANO HII HAINA MAANA YOYOTE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…