Dr Slaa, Tindu Lisu, Kubenea na Mengi tuwape tuzo gani?

Watanzania

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2009
Posts
727
Reaction score
44
Kama kuna watanzania wanaostahili tuzo kwa mchango wao katika taifa hili baada ya kifo cha baba wa taifa basi ni Dr. Slaa, Tindu Lisu, Kubenea na Mengi. Hawa wamediliki kupambana na rushwa ya kiwango cha ufisadi bila woga wowote hata kwa kuhatarisha maisha yao na mali zao dhidi ya umafia unaoweza kufanywa na Mafisadi. Sote tunajua mambo waliyofanya.

Dr. Slaa na Tindu Lisu ni watanzania wa kwanza kutaja majina 11 ya watu wa kuzomewa kwa sababu ya ufisadi wao. Gazeti la Kubenea ndilo pekee lililotaja majina yote 11 na tuhuma zinazowakabili. Kwa upande wake Mengi alitaja majina ya mafisadi papa. Lakini je nani atawapa tuzo hawa watanzania wenzetu? Na nani wa kutoa tuzo hili? Asasi za kiraia za Tanzania au tusubiri ubalozi wa Marekani?. Lakini kwa hakika wanastahili tuzo la ujasiri wa kupenda nchi. Wanapotokea kwa mfano watu wanaotaka sifa wasizostahili kama Kafulila ni wa kupuuza tu.

Wapo wengine pia wanostahili tuzo. Watanzania hatunabudi kutambua mchango wa pekee kwa aliyeanzisha JF. Amefanya kitu kikubwa sana katika maisha. Pia Mzee Mwanakijiji ametoa mchango mkubwa katika harakati za kuleta usawa katika nchi yetu. Tuwatunze tukiwa nao bado.
 
ok Watanzania sijui nani mwingine anastahiri pongezi !
 
Kwani umesikia watakufa unasema tuwatunze tukiwa nao bado sasa Watanzania sijui una maana gani hapo... niweke sawa nikupe yangu maoni
 
FirstLady1 baada ya kifo cha baba wa Taifa hawa watu wamenigusa sana. Wengine pia wametoa michango yao lakini hawa ujasiri wao ni wa pekee. Kabla ya kifo cha baba wa Taifa Katabalo aliyekuwa mwandishi gazeti la Mfanyakazi wakati wa utawala wa Mh. Mwinyi naye alinigusa sana, nasikitika naye ameondoka bila kupewa tuzo kwa kutetea nchi yetu.
 
Kwani umesikia watakufa unasema tuwatunze tukiwa nao bado sasa Watanzania sijui una maana gani hapo... niweke sawa nikupe yangu maoni

Sina maana hiyo, naona ni vyema watu wakapata tuzo muda muafaka. Tutambue michango ya watu mapema. Mwalimu Nyerere kwa mfano umuhimu wake umeonekana zaidi wakati hatunaye. Kumbe tungetambua mapema tungefaidika zaidi kwa kumsikia.
 
Tuzo kubwa kwao ni sisi nasi kuwaunga mkono kwa kupambana na ufisadi bila kificho wala woga. Kusimama na kusema wamefanya makubwa bila kuwaunga mkono ni kama kuwakatisha tamaa.
 
Kama kuna watanzania wanaostahili tuzo kwa mchango wao katika taifa hili baada ya kifo cha baba wa taifa basi ni Dr. Slaa, Tindu Lisu, Kubenea na Mengi. Hawa wamediliki kupambana na rushwa ya kiwango cha ufisadi bila woga wowote hata kwa kuhatarisha maisha yao na mali zao dhidi ya umafia unaoweza kufanywa na Mafisadi. Sote tunajua mambo waliyofanya.

Dr. Slaa na Tindu Lisu ni watanzania wa kwanza kutaja majina 11 ya watu wa kuzomewa kwa sababu ya ufisadi wao. Gazeti la Kubenea ndilo pekee lililotaja majina yote 11 na tuhuma zinazowakabili. Kwa upande wake Mengi alitaja majina ya mafisadi papa. Lakini je nani atawapa tuzo hawa watanzania wenzetu? Na nani wa kutoa tuzo hili? Asasi za kiraia za Tanzania au tusubiri ubalozi wa Marekani?. Lakini kwa hakika wanastahili tuzo la ujasiri wa kupenda nchi. Wanapotokea kwa mfano watu wanaotaka sifa wasizostahili kama Kafulila ni wa kupuuza tu.

Wapo wengine pia wanostahili tuzo. Watanzania hatunabudi kutambua mchango wa pekee kwa aliyeanzisha JF. Amefanya kitu kikubwa sana katika maisha. Pia Mzee Mwanakijiji ametoa mchango mkubwa katika harakati za kuleta usawa katika nchi yetu. Tuwatunze tukiwa nao bado.

Mkuu,Asante kwa post nzuri ila mimi nafikiri anyesathili tuzo hapa nia Dr Slaa hawa wengine wamefany nini hadi kustahili tuzo?
 
Mengi apewe tuzo?????

Chizi apewe rungu??????
 
tuzo kubwa ni kwako mwananchi kukataa UFISADI kwa sauti moja.
 
Back
Top Bottom