Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
Kama kuna watanzania wanaostahili tuzo kwa mchango wao katika taifa hili baada ya kifo cha baba wa taifa basi ni Dr. Slaa, Tindu Lisu, Kubenea na Mengi. Hawa wamediliki kupambana na rushwa ya kiwango cha ufisadi bila woga wowote hata kwa kuhatarisha maisha yao na mali zao dhidi ya umafia unaoweza kufanywa na Mafisadi. Sote tunajua mambo waliyofanya.
Dr. Slaa na Tindu Lisu ni watanzania wa kwanza kutaja majina 11 ya watu wa kuzomewa kwa sababu ya ufisadi wao. Gazeti la Kubenea ndilo pekee lililotaja majina yote 11 na tuhuma zinazowakabili. Kwa upande wake Mengi alitaja majina ya mafisadi papa. Lakini je nani atawapa tuzo hawa watanzania wenzetu? Na nani wa kutoa tuzo hili? Asasi za kiraia za Tanzania au tusubiri ubalozi wa Marekani?. Lakini kwa hakika wanastahili tuzo la ujasiri wa kupenda nchi. Wanapotokea kwa mfano watu wanaotaka sifa wasizostahili kama Kafulila ni wa kupuuza tu.
Wapo wengine pia wanostahili tuzo. Watanzania hatunabudi kutambua mchango wa pekee kwa aliyeanzisha JF. Amefanya kitu kikubwa sana katika maisha. Pia Mzee Mwanakijiji ametoa mchango mkubwa katika harakati za kuleta usawa katika nchi yetu. Tuwatunze tukiwa nao bado.