Elections 2010 Dr.slaa tunahitaji mwongozo wako tuko njia panda

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
4,780
Reaction score
3,227
Kuanzia jana jioni tuliona faraja baada ya kuanza kutoka matokeo ya Urais, ubunge na udiwani toka vituo mbalimbali.Kulingana na sheria tuliyosoma ya uchaguzi uchaguzi inaeleza wazi kuwa" kura zote zitahesabiwa vituoni na hata wasimamizi wasaidizi walifanya home work yao kwa kuzingatia sheria hiyo.

Mwanzo wa kutangaza matokeo toka sehemu mbalimbali hatukusikia kama wasimamizi walifanya makosa kutangaza.Leo kumekucha Watanzania wakitegemea matokeo yataendelea kutangazwa kama kawaida.Cha ajabu sasa tunaanza kusikia taarifa mpya kuwa matokea yalikuwa yakitangazwa sivyo.

Kwa kuwa Watanzania tumeanza kuwa na wasiwasi na sheria hii isiyo rasmi iliyoanza leo kama kweli na agizo halali:

Tunamuomba Dr.SLAA na wagombea wengine wa urais wawajulishe kama hakuna uvunjifu wa sheria hapa, yeye kama mgombea ana haki ya kuhoji na kutujuza sisi tulipiga kura zetu.

Ikumbukwe kuwa kura hizi tuna haki nazo ni mali yetu, mpaka pale mshindi atakapotangazwa.

Ni muda muafaka sasa kwa Mheshimiwa shimbo kutoka mbele na kukemea hii hali kama alivyofanya mwanzo kwani uvunjifu wa amani unanukia hapa.

Tunaanza kupata taarifa kuwa huko zanzibar yameanza ya 1995,2000 na 2005
TUNAELEKEA WAPI????????? WATANZANIA TUSIKUBALI AMANI TUNAANZA KUIWEKA REHANI. CHONDE CHONDE WAGOMBEA TOENI KAURI, MSISUBIRI DAMU IMWAGIKE.

KAMA ALIVYOKWISHA KUSEMA DR.SLAA KUWA WATAKAOSABABISHA DAMU KUMWAGIKA NI CCM SASA WATANZANIA TUKATAE.TUPAZE SAUTI KUPITIA VIONGOZI WETU DUNIA ISIKIE.
 
Sijui lini wazanzibar watapata kuongozwa na wanaemtaka
 
kwa kweli hili linatupa wasiwasi sana tunakosa imani nao tunashindwa kuelewa sababu maalum yakufanya matokeo hayo yasitangazwe au ndio wako kwenye harakati ya kuyapindua hivi ni lini viongozi wa africa/ tanzania wataweza kuwa wa kweli na wa wazi kwa wananchi wao mana wanajisahau kabisa kuwa mwananchi nae ana haki ya kujua kila jambo linalomuhusu. jamani tuwe macho tusije tukapigwa changa la macho tukijiona!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…