Silaa tafadhali kutaka kwako kura kusikufanye ukatunyang"anya tonge wafanyakazi mdomoni. Tunazitaka sana hiyo nyongeza ya mshahara no matter imetangazwa wapi? we mbona umeahidi mengi? hizo ahadi si rushwa na si kinyume na maadili ya kampeni? kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni ulizitaka kura zetu na ukaahidi kuongeza mshahara hiyo si rushwa? Nilikupenda sana niliapa kutopiga kura mwaka huu lakini ulipokuja wewe nikahamasika lakini kwa hili unaniboa na kinirudisha kulekule. Wafanyakazi hatudanganyiki na nyongeza ya mshahara hata akiongeza kama hatukumtaka tusimgempa na hata kama asipoongeza kama tulimtaka tungempa. NImegundua kuwa wagombea wote wapo kwaajili ya kura tu na wala si maslahi ya wananchi, kama kweli unamaslahi nasi ungeacha wafanyakazi mwezi huu wa nane japo tufikie hiyo 175,000/= tupambane na maisha. Khaa bee!!!!
Dada,
Tatizo ni kwamba wewe hukutazama - kwa umakini - hotuba ya Dk. Slaa alipozindua kampeni pale Jangwani, Jumamosi, au hukutazama kabisa.
Unacholalama kinatokana na DISINFORMATION CAMPAIGN inayoendeshwa na vyombo vya habari vilivyonunuliwa na CCM, kupotosha kila kilichosemwa na Dk. Slaa. Naomba nikufahamishe:
1. Slaa amesema kwamba CHADEMA haitoi ahadi ya kupandisha mishahara, kufikia Shs 350,000/- kama HONGO kwa wafanyakazi, amesema kwamba ni HAKI ya wafanyakazi kupata kiwango hicho cha mshahara.
2. Slaa ametamka wazi kwamba suala la maslahi ya wafanyakazi, hata kiwango hicho cha chini, ni suala ambalo lina muda mrefu, kwa sasa ni miaka nne, si suala geni.
Kwa hiyo dada, tafakari kwanza kabla ya kubwata (umebwata bila kuwa na uhakika wa unachokisema). Kumbuka, wako watu wengi sana wanaosoma kurasa hizi pepe... zaidi ya wanachama milioni 4... wengi wao wenye uwezo wa kutoa maamuzi mazuri na mabaya kwetu sote. Hata Mkuu wa Nchi naye ni mwanachama humu ndani, na anasoma tunachoandika, anakifanyia kazi.
JK alisema Serikali yake HAIWEZI - nilisikiliza hotuba yake siku hiyo - kupandisha mishahara, hata kama wafanyakazi wakigoma miaka nane, na alisema "kama ni kukosa kura, niko tayari kuzikosa..." Hana haja na kura za wafanyakazi.
Sasa bora mumpe tu Slaa, ambaye amesema anahitaji kura zenu, na kwamba CHADEMA itakuwa na uwezo wa kupandisha mishahara pamoja na kuweka mazingira bora zaidi ya kazi.
Una cha zaidi cha kukusumbua, tukutoe dukuduku lako?
-----> Mwana wa Haki
Njia nyeupe mbele kwa mbele hadi Ikulu. Uchafuzi wa CCM ni mtaji wa CHADEMA. Wakichafua, wananchi wanachukia, wanaipa kura CHADEMA!
People's Power! Hatudanganyiki!