Ni muhimu sana kwa CHADEMA kuwatumia wale wabunge wailopata yale majimbo tunayoyaita HOT-CAKE kama vile Ubungo, Kawe, Arusha, Mbeya, Moshi na yale ya mwanza ili utendaji wao uwe ni mfano kwa wale waliochagua kutoipigia kura CHADEMA au kutokupigakura kabisa (kwa sababu ya kutokuwaamini au kutokujua) ili next-time wajue kuwa kupanga ni kuchagua na chama makini kweli ni CHADEMA.
Pia kwa wale ambao hatujajiingiza kwenye wajibu wa chama mojakwamoja kwa sababu ya muda na mambo mengine basi tutumie busara zetu kuwaelimisha watanzania wenzetu katika kipindi cha miaka mitano mpaka 2015 ili waweze kupiga kura (wasisuse) kama walivyo fanya sasa. Hii itasaidia pale ambao ukiwa na petroli ya lita elfu kumi ukataka kuichachua kwa mafuta ya taa ya lika elfu moja au mbili basi inakuwa ni ngumu kitu ambacho hakitoleta matunda yaliyokusudiwa kwa wale waizi wa kura!.