Wana jukwaa,habari nilizozipata kutoka kwa katibu mwenezi jimbo la Segerea,ni kwamba kesho katibu mkuu wa CDM Dr W Slaa ataongoza mkutano wa hadhara wa mabaraza ya katiba katika majimbo matatu ya mkoa wa Dar es Slaam.mikutano hiyo ya kesho tarehe 24/08/2013 itaanzia jimbo la Kigamboni asubuhi,kisha atakuwa jimbo la Segerea mnamo saa saba mchana.akiwa jimbo la Segerea mkutano mkubwa utafanyika ktk kiwanja cha msikate tamaa,kilichopo karibu na shule ya msingi ya Vingunguti,ambayo ipo kata ya Vingunguti.mnaalikwa watu wote wapenda mabadiliko kuhudhuria mkutano huo.mh Mdee,Mnyika,Mabere Marando na wengine wengi watakuwepo kuuhutubia umma wa watanzania.baada ya hapo Dr atakwenda jimbo la Ukonga ambako atahitimisha mikutano ya kesho.
Naomba kuwasilisha.
Naomba kuwasilisha.