Drake aingia kwenye rekodi kwenye chati za Billboard na album yake ya "Views"

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Drake hakamatiki kwa wasanii wa Hip Hop wa kizazi hiki – albamu yake ‘Views’ yaingia kwenye rekodi ya orodha ya albamu zilizowahi kukaa muda mrefu kwenye chati za Billboard.

Albamu hiyo iliyotoka mwezi Mei mwaka huu, imekaa kwenye nafasi ya tano bora ya chati za Billboard Top 200 kwa wiki 26. Mpaka sasa ni albamu sita pekee ndio zimeweza kuweka rekodi hiyo tangu mwaka 1963 ikiwemo albamu ya Adele “21” iliyoongoza kukaa kwenye chati hizo kwa wiki 39.

Wasanii wengine waliowahi kuweka rekodi hiyo ni pamoja na “Bad” ya Michael Jackson iliyokaa kwa wiki 38, “Songs in the Key of Life” ya Stevie Wonder ilikaa kwa wiki 32, “The Bodyguard Soundtrack” ya Whitney Houston ilikaa 30.

Mpaka sasa albamu hiyo imefanikiwa kuweka rekodi kadhaa ikiwemo ya kusikilizwa mara nyingi zaidi kwenye mtandao wa Apple Music ikiwa ni mara bilioni 1 na kusikilizwa zaidi ya mara milioni 880 kwenye mtandao wa Spotify.

MY TAKE: Kuna ambaye ameshasikiliza album ya drake atupe hint kua whats so special in that album hadi inakuja kasi sana.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…