DRC: Mgonjwa wa pili wa Ebola afariki dunia

DRC: Mgonjwa wa pili wa Ebola afariki dunia

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Ebola.JPG

Mgonjwa wa pili aliyekuwa anaugua Ugonjwa wa Ebola amefariki dunia huko Kaskazini Magharibi mwa DRC.

Taarifa hiyo imetolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ikiwa ni siku chache baada ya mlipuko mpya wa ugonjwa huo kutokea DRC.

WHO imesema uchunguzi wa vinasaba ulionesha maambukizo mapya yalithibitishwa wiki iliyopita kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa.

Hata hivyo, maambukizo hayo hayahusiani na mlipuko wa mwisho, ambao ulitangazwa mwezi Desemba, 2021.

Mgonjwa wa pili alikuwa ni mwanamke na ndugu wa mgonjwa wa kwanza. Mgonjwa huyo alianza kuonyesha dalili za Ebola mnamo Aprili 5, 2022 lakini hakupata matibabu kwa zaidi ya wiki moja. Baadaye alilazwa katika kituo cha wagonjwa wa Ebola mjini Mbandaka na kufariki siku iliyofuata.

Source: DW
 
Back
Top Bottom