DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,149
Reaction score
3,963
DRC ndani ya EAC: Nini maana yake?

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo wanatarajia kukubali Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama wake wa saba katika mojawapo ya matukio yenye maana kubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii katika eneo la Maziwa Makuu.

DRC - ikiwa na watu takribani milioni 92, litakuwa ndiyo taifa lenye watu wengi zaidi miongoni mwa nchi wanachama na kutaifanya EAC sasa kuwa jumuiya yenye soko la takribani watu milioni 260. DRC ni kubwa kieneo na inapakana na takribani nchi tano wanachama wa jumuiya hiyo - kwa maana ya nchi zote kuondoa Kenya. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini.

Hatua hiyo ya wakuu wa EAC kupitia mkutano wao utakaofanyika kwa njia ya mtandao leo, ni hitimisho la safari ya takribani miaka 10 - iliyoanza wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila na kuhitimishwa kwa zoezi la uhakiki lililoongozwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Peter Mathuki, kati ya Juni na Julai mwaka huu.

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Rais Felix Tshisekedi wa DRC ameonyesha hamu kubwa ya taifa lake kujiunga na jumuiya hiyo na alitumia sehemu kubwa ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa taifa lake mwaka huu kueleza namna taifa lake lilivyokuwa tayari kuwa mwanachama mpya wa EAC.

Kwanini Tshisekedi na Wakongomani wana hamu ya kujiunga muungano huu?

Jiografia
Kijiografia, hakuna nchi nyingine yenye sifa ya kuwa mwanachama wa EAC kuizidi DRC. Mojawapo ya masharti ya mwanzo ya kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo yalikuwa kwamba nchi ni lazima iwe inapakana na mojawapo ya nchi wanachama lakini taifa hili mashuhuri duniani linapakana na nchi zote wanachama.

Kuondoa ujirani mwema huo, Wakongomani ni kama vile walikuwa wanachama wa EAC hata kabla ya nchi yao kuwa mwanachama rasmi wa jumuiya. Kwa mfano, kwa muda mrefu, DRC ilikuwa inaongoza kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake kuliko nchi wanachama, muziki wenye asili ya taifa hilo ukiwa mashuhuri katika nchi zote za Afrika Mashariki na watu wake mbalimbali wakiweka makazi yao ya kudumu katika nchi tofauti inazopakana nazo.

Je, DRC inaweza kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika MMashariki

Miongoni mwa nchi wanachama wa EAC, pengine hakuna taifa ambalo watu wake wametapakaa katika nchi zote za jumuiya hiyo - Wakongomani wakijulikana kwa tabia yao ya kutoogopa kutafuta riziki popote nje ya taifa lao - tofauti na wananchi wa baadhi ya nchi wanachama wengine ambao si watu wa kuhangaika duniani kutafuta maisha.

Kwa sababu hiyo, kijiografia na kiutamaduni, DRC ilikuwa mwanachama wa EAC miaka mingi kabla hata haijapata fursa hii ya kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa sita.

Wakati jumuiya ikionekana kuzidi kutanuka, ni vigumu kuona taifa lingine litakalokuwa na "wenyeji wengi walio wageni "kuzidi ujio huu wa taifa lililokuwa likijulikana kama Zaire wakati wa utawala wa Mobutu Sesesseko.

Uchumi
Kwa sasa, Pato la Nchi Wanachama wa EAC linafikia kiasi cha dola bilioni 193 na ujio wa DRC utaongeza pato hilo kwa dola bilioni 50 zaidi kufikia dola 240. Hiki ni kiwango kikubwa kuongezwa na nchi moja katika eneo la dunia linalofahamika kwa umasikini mkubwa.

Lakini siri kubwa iko katika soko. Kwa sababu ya matatizo mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, DRC inaonekana kama nchi ambayo bado fursa zake hazijatumiwa ipasavyo na wananchi wake lakini pia na nchi Jirani.

Hata kabla ya kuiruhusu DRC kuingia EAC, viongozi wa juu wa nchi wanachama kama vile Uhuru Kenyatta, Paul Kagame na Yoweri Museveni wameonekana kujisogeza karibu na Tshisekedi.

Kuna mpango wa Afrika wa kuunganisha upande wa Mashariki na Magharibi - kutoka Bahari ya Hindi hadi Atlantic na DRC ni mojawapo ya nguzo muhimu kwenye jambo hilo kubwa.

Kuna mpango wa kujenga barabara kupitia mradi wa TAH8 unaounganisha bandari ya Mombasa, Kenya kwenda katika jiji la Younde, Cameroon na kisha Atlantic. Hizi ni mojawapo ya miradi mikubwa ya miundombinu barani Afrika inayotazamwa kwa jicho la kipekee na Umoja wa Afrika.

Rais Museveni amewahi kuzungumza huko nyuma kwamba tatizo kubwa la Afrika ni ukosefu wa masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi na ujio wa taifa lenye watu milioni 92 unamaanisha soko kubwa kwa bidhaa za nchi wanachama wa EAC.

Usalama
Mara zote ukubwa wa DRC umekuwa na changamoto za kiusalama kwa nchi wanachama. Rwanda na Uganda zimekuwa zikisumbuliwa na makundi ya waasi yanayojificha katika misitu minene ya DRC. Lakini pia nchi hizo mbili zimewahi kupigana zenyewe ndani ya taifa hilo kwa sababu ya kuwania kuwa na ushawishi kwa viongozi wa DRC.

Ni matarajio ya viongozi wa EAC kwamba kuwa na DRC ndani yao kutasaidia kujenga mipango itakayowezesha urahisi wa kudhibiti vikundi vya waasi na ugaidi lakini pia kufanya biashara kwa Pamoja badala ya kudhulumiana.

Kuna dhana kutoka katika baadhi ya jamii ya Wakongomani kwamba Rwanda na Uganda wamekuwa wakitumia utajiri wa taifa lao kwa faida yao kwa kutumia visingizio vya kiusalama.

Amani ya kudumu katika eneo la maziwa makuu itasababisha viongozi wa nchi husika sasa kutumia nguvu zaidi katika kujenga uchumi na ushirikiano badala ya kupanga namna ya kufanya uvamizi au kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi au uasi kupora mali za DRC.

Ndoto ya Waasisi
Hatua ya DRC kuingia EAC inachukuliwa pia kama kutimia kwa ndoto za waasisi wa siasa za Umajumui wa Afrika walioamini kwamba namna pekee kwa Afrika kusonga mbele ni kwa kuwa na umoja wa kisiasa na kiuchumi miongoni mwao.

Wakati Tshisekedi akitaka DRC iingie EAC, alikuwa anatimiza ndoto za Patrice Lumumba, Julius Nyerere, Milton Obote na Jomo Kenyatta. Ni matarajio ya wachambuzi wa masuala ya ushirikiano kwamba muda si mrefu nchi kama Somalia, Congo Brazaville na Ethiopia nazo zinaweza kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.

Kwa kufanya hivyo, nchi wanachama wa EAC wanaweza kuwa na uwezekano wa kuwa na kura moja kwenye masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa eneo la Maziwa Makuu na Afrika kwa ujumla - bila kuzingatia tofauti za lugha wanazozungumza.

Ni jambo zuri kwamba Museveni ambaye ndiye kiongozi mwenye ari zaidi ya mtangamano wa Afrika yuko madarakani bado na jambo hili linaendana na ndoto zake za muda mrefu za kuunganisha Afrika kwa mafungu.

Changamoto
Takribani miaka 10 iliyopita, Sudan Kusini iliingia EAC kwa mbwembwe na furaha kubwa. Wengi walitaraji makubwa kutoka katika taifa hilo. Hata hivyo, kuwepo kwake kwenye jumuiya hakuonekani kupunguza chochote kwenye migogoro na sintofahamu miongoni mwa vinara wakuu wa taifa hilo.

Kimsingi, hakuna mijadala inayofanyika au jitihada za makusudi zinazofanywa na EAC kuhakikisha nchi hiyo mwanachama inakuwa na amani ya kudumu.

Kwa maneno mengine, kuwa kwake mwanachama wa jumuiya hakujaondoa tofauti zake za ndani na hakujaongeza uwezekano wa nchi wanachama kusaidia kuondoa matatizo yake.

Hili ndilo swali ambalo wachambuzi wanajiuliza sasa kwamba kama DRC itakuwa tofauti na italeta kinachotarajiwa na wengi baada ya kujiunga kwake na EAC. Kama ilivyokuwa kwa akina Salva Kiir na Riek Machar huko nyuma, Tshisekedi anaonekana kuwa na nia na ari kubwa - tatizo ni kwamba haijulikana EAC iko tayari kiasi kuisaidia DRC kusimama vizuri.

Changamoto nyingine kubwa kuhusu DRC inahusu dhamiri za ndani za baadhi ya viongozi wa EAC kuhusu kuwa na taifa hilo jipya kama mwanachama. Kuna nchi zinaitazama Kongo kama taifa la kuibiwa - shamba la bibi, na haijulikani kama tabia hiyo itaondoka au itamea zaidi kupitia muungano huu.

Tayari baadhi ya viongozi wa nchi za EAC wamefanya ziara kwa Tshisekedi kufanya dili kwa ajili ya nchi zao hata kama ya tukio la leo. Ipo hatari ya uhakika kwamba huenda maslahi ya baadhi ya nchi yakagongana huko mbele ya safari na hatimaye nchi zikajikuta zinarudi palepale zilipokuwa awali.

Lakini, leo ni siku ya kusherehekea kuikaribisha DRC ndani ya EAC.
 
Hata Sudan ya Kusini iliingia kwa mbwembwe ikijua ndio mwisho wa Matatizo yake ya ndani. Lakini leo Ni Zaidi ya miaka 10 tangu Sudan ya Kusini ijiunge na EAC lakini bado Vita imepamba Moto.
Kongo ni tofauti sana na s.sudan
Kasome kwanza shida ya kongo iko wapi???ukishaelewa rudi hapa anko
 
Karibu Kongo, taifa lenye watu zaidi ya milioni 90 na lenye ukubwa wote huo, ni dhahiri ni fursa nzuri sana kwa watakaojituma na kuacha kulialia au kusuburi embe lidondoke kutoka kwenye mwembe, mivivu itaendelea kulalamika milele.

Kuhusu amani Sudan Kusini ni tofauti sana, wale kule nimeishi kwao miezi mitatu na kuona walivyo, wengi wametokea maporini walikoishi maisha ya vita vita, kisha wakabuni taifa, kwa hivyo kuwabadilisha sio kazi ndogo, yaani hata maofisini wanavyofanya kazi full ubabe na kufanyiana ukatili, itawachukua muda sana.

Bakongoman ni watu wa kujituma, tuko nao Kenya wanafanya biashara kote, Wakenya tutiririke huko na kusaka fursa maana zipo nyingi. Haya maupumbavu ya kufungiana hukwamisha sana, na ndio kitu mama Samia amejaribu kufungua kwa Tanzania, sema Watanzania kwa walivyo waoga bado wenyewe hawajamuelewa.

Kufungiana huwa kunalemaza shughuli za kiuchumi, unakuta leo Mtanzania na Mkenya mkikaa muwaze kufanya jambo kwa ubia, yaani hata kutembeleana kwenyewe ni shughuli, vikwazo vya kufa mtu.
 
maana yake ni kwamba EAC makes much more economic and geopolitical sense to them than SADC given the different points of interactions and entanglements with Rwanda and Uganda

for Kenya it will provide a bridge to the francophone central Africa region which is a key pillar in Kenya's geopolitical and economic goals.

I don't think it changes much for Tanzania besides more access to that market... ditto South Sudanand Burundi. I am open to be corrected on this
 

What interests me more is the belt between Mombasa port all the way to Atlantic ocean.
 
Mentality za kutawaliwa ki-chifu chifu bado zimemganda Mwafrija kama luba. Kila kitu ni wazo la Rais. Congo na umajumui wa EAC unamhusu Tshisekedi, Nyerere, Obote na Kenyatta. Watu ambao walishindwana wakavunja EAC, na wakapigana vita ma-nchini mwao kwa sababu za kikabila, udikteta, na kugombea madaraka. Lakini bado tunawatukuza. Li-muungano la Nyerere nchini mwake kwenyewe mpaka kesho bado ni utata mtupu kwa sababu ya kutaka kuunganisha watu bila ridhaa yao.

Na Museveni kuwa ni jambo jema kuweko madarakani hayo ni mawazo yako wewe! Dunia nzima inakesha ikifunga na kusali Museveni aondoke.

Hii mitawala ya Afrika sio miungu watu na sio machifu. Nchi au jumuia ya watu milioni 200 haiwezi kuongozwa na akili za kichwa kimoja au vichwa vinne. Usitudanganye danganye hapa na visababu dhaifu vya kufurahia ujio wa Congo EAC. Leo ni siku ya kusherehekea, tusherehekee nini wakati wewe mwenyewe umesema kuna matatizo kibao ya EAC ? Unasherekea ukidhani ni fursa kuibaka Congo?
 
Hata Sudan ya Kusini iliingia kwa mbwembwe ikijua ndio mwisho wa Matatizo yake ya ndani. Lakini leo Ni Zaidi ya miaka 10 tangu Sudan ya Kusini ijiunge na EAC lakini bado Vita imepamba Moto.
Hakuna vita South Sudan wacha bangi wewe.
 
"I don't think it changes much for Tanzania besides more access to that market... "

DRC tupo nao miaka na mikaka kama wateja wetu muhimu kama jirani na SADC member
 
yes! joining Indian Ocean to the Atlantic has not only been a major goal for Kenya but AU
Pipe dreams.

You will link msa to Atlantic kupitia wapi? Hadi mfikie Congo mnajua mtapita wapi?

FYI, tunafika Atlantic soon via congo-zambia-Namibia. Railway line already in place from lobito port to Congo. We are finalizing to link railway to karema port then we will reach Congo.

While you are dreaming about it, we (TZ) are already at it. Kunyaland still have more issues to catch up... TZ ndio inatemgeneza mazingira ya ukanda huu.. Very calculated moves.. Congo tumemleta sisi, same to Burundi and Rwanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hakuna Vita Ni vipi hizo kambi za wakimbizi zisifungwe hapo Kenya na kule Uganda? Au mnamega Mifedha ya UNHCR?
Ukijua tofauti kati ya peace keeping iliyoko Sudan na peace forcing iliyoko Congo utajua kama kuna vita au lah!
 
Sioni utofauti wowote. As long as madini bado yapo kamwe migogoro yake haitokaa iishe..
DRC haiwezi kuondokana na Matatizo yake ya ndani kwa kujiunga na EAC.

EAC haina Manfesto ya kuingilia Mambo ya ndani ya nchi husika. Viongozi wanalindana na kuogopa kukosoana. Ni tofauti na Umoja wa Ulaya (EU) ambayo Nchi Mwanachama inabanwa endapo itakiuka Misingi ya EU. Pia EU husaidia kwa Hali na Mali nchi Mwanachama endapo itakumbwa na Matatizo ya Kiuchumi au Kijamii. Mfano Mdogo Ni Jinsi UJERUMANI ilivyotumia Mabilion ya EURO ambazo Ni za walipa Kodi wa UJERUMANI kuokoa uchumi wa UGRIKI na CYPRUA. Isingelikuwa UJERUMANI Basi Madeni yangelizisambaratisha nchi za UGRIKI na SYPRUS.

Huku kwetu tunafungiana hata kuuziana Mahindi na Mitungi ya Gas harafu eti tunajiita Jumuia, HIKI Ni kichekesho Cha Karne.
 
Porojo miiingiii...
 
Sisi hatuna common interest.
Wale wana common interest.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…