DRC: Rais avunja muunganiko kati ya wafuasi wake na wale wa Rais Kabila

DRC: Rais avunja muunganiko kati ya wafuasi wake na wale wa Rais Kabila

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema anavunja ushirikiano wa kisiasa baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono-CACH, na vile vilivyo upande wa mtangulizi wake, rais mstaafu Joseph Kabila-FCC.

Ushirikiano huo umekuwa ukiongoza serikali ya Kongo kwa miaka miwili iliyopita, Kabila akilidhibiti bunge, huku Tshisekedi akiwa na mamlaka ya rais. Uamuzi huo Tshisekedi ameutoa katika hotuba kwa taifa jana Jumapili.

Hotuba yake rais Tshisekedi ilikuwa ikisubiriwa kwa shauku, baada ya mazungumzo ya mashauriano aliyoyafanya mwezi novemba, kwa kile kilichoelezewa kuwa lengo la kuunda muungano wa taifa.

Katika hotuba hiyo, Tshisekedi ameyagusia masuali mengi ambayo amesema yalijitokeza katika mazungumzo hayo, la muhimu zaidi likiwa ni hatua za kuhitimisha ushirikiano baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono yeye, maarufu CACH, na ule wa vyama vilivyo upande wake rais mstaafu Joseph Kabila yaani FCC.
 
Watawala wa Africa wanafanana ,yaani ukisikiliza siasa za Tanzania ni kama Kongo,ukisikiliza siasa za Uganda ni kama Rwanda yaani ni kama laana.
 
Watawala wa Africa wanafanana ,yaani ukisikiliza siasa za Tanzania ni kama Kongo,ukisikiliza siasa za Uganda ni kama Rwanda yaani ni kama laana.
Acha kufananisha Tanzania na vitu vingine🤪🤪🤪🤪🤪🤪
 
Hii tabia ya kumuingiza mtu madarakani kwa figisu kisha unataka wewe ndio tena utawale kwa remote ni ya kipumbavu kabisa.

Kabila aliishaondoka madarakani baada ya kukaa miaka 17 tena baada ya kuzidisha miaka miwili zaidi, bado tena anataka nini.

Wasimruhusu arudi tena madarakani, Congo ina zaidi ya raia milioni 80 na wapo wengi tu wenye uwezo wa kuongoza, yeye astaafu salama kwani amefanya ufisadi mkubwa ktk utawala wake.
 
Rais Wa Ghana, Mh Nana Akufo-Addo sio "MUAFRIKA HALISIA". Haiwezekani akawa Muafrika. Anatakiwa afukuzwe Afrika aende akatafute taifa lake au akatafute HIFADHI huko Brazil, Visiwa Vya Haiti, Marekani au Ulaya.

Yani mpaka siku ya jana 07/12/2020 nchi ya Ghana ilivyopiga "KURA YA URAIS" hakuna hata "MGOMBEA MMOJA WA UPINZANI ALIEKATWA JINA LAKE", wala hakuna "FIGISU FIGISU" zilizofanywa na serikali yake wala polisi. Hakuna hata "MTU MMOJA ALIEKUFA, ALIEUMIZWA WALA KUFUNGWA GEREZANI" kwa kupigwa na polisi wala jeshi kwa muda wote kuanzia kampeni zilivyoanza mpaka kupiga kura.

Hivi huyu Rais Nana Akufo-Addo ni Muafrika halisia kweli???
Yeye nani mpaka kuendesha kampeni na uchaguzi kwa "AMANI NA UHURU" kiasi hicho??? Yani kaendesha kampeni na uchaguzi bila hata "KUUA WALA KUUMIZA WALA KUFUNGA" yoyote gerezani??? Basi hata "KUMTIA ULEMAVU" mfuasi mmoja wa upinzani ameshindwa???.

Anajiona yeye ni "SPESHO SANA" kufuta "MILA ZETU ZA KIAFRIKA ZA UCHAGUZI"??? Ameshindwa kujifunza kwa Tanzania, Zanzibar, Uganda, Kenya au hata huyo Rais Wa Congo njia walizopita na wanazopita ili "KULINDA NA KUENZI MILA" zetu za kiafrika kwenye maswala ya Uchaguzi???.

"ANATAKIWA AKEMEWE VIKALI SANA NA MATAIFA YOTE YA AFRIKA. AMETUDHALILISHA WAAFRIKA"!!!!!
Bila kukosea Ghana ndiyo nchi inayo ongoza kuwa na demokrasia nzuri humu Africa kwahiyo wengine mtasubili sana, jana nimetizama kwenye vituo vya kupigia kura kuna viti kabisa tena vya plastic, wakifika wanakaa kabisa, mwenzio akinyanyuka unasogea sasa hiyo kwetu sijui mwaka 3000 labda
 
Kaona anaongozwa yy badala ya kuongoza aisee,acheze gemu vizuri la sivyo yatamtokea ya mdomoni,siasa za Kongo ni ngumu sana kama ilivyo kwa nchi nyingine za kiafrika na kuna tego kubwa lipo pembeni yake akileta masihara atalikwaa kabisa,kabila ashafura huko kwa hasira,Mr slim naye anaona ndege atamkimbia nao sasa wanapanga mikakati yao,mungu awasaidiea aisee Congo ni taifa kubwa sana afrika lakini siasa hiziii ndo mana alisema babu yangu kuwa "baada ya shetani anayefuata kuingia Motoni ni mwanasiasa"
 
Hivi Kagame yupo upande wa Kabila au Tshekedi?
 
Back
Top Bottom