bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Democratic Republic of Congo zamani Zaire kama nchi wanapitia kipindi kigumu kwa sasa kutokana na Waasi wanaojiita M23 kuendesha vita nchini humo na kufikia kuteka baadhi ya miji muhimu.
Pamoja na kuwepo wanajeshi walinda amani wa kila aina kuanzia wale wa UN mpaka SADC bado hali imeendelea kuwa tete DRC mpaka unajiuliza tatizo lipo wapi.
Kumbe basi unagundua DRC hawahitaji kuwa na wanajeshi kutoka mataifa mbalimbali, bali wanahitaji kusaidiwa kuwa na jeshi lenye uzalendo na nchi yao, imara, lenye upendo, wenye mafunzo ya kutosha pamoja na nidhamu ya hali ya juu kwani nidhamu ndo kila kitu jeshini, pamoja na maslahi mazuri.
Kwa kuangalia wale wanajeshi waliotekwa/kujisalimisha Goma unagundua mambo mengi sana kama vile ukosefu wa uzalendo pamoja na morali, nidhamu, kukata tamaa, maslahi duni kwani baadhi yao hawana hata uniform za kijeshi na medani finyu za kivita.
DRC wana uwezo wa kufanya hayo yote labda kusaidiwa wataalamu tu kwani wana faida kubwa ya population, wana resources za kutosha na adimu duniani ambazo wakizitumia vizuri kwa kuziuza watakua na uwezo wa kununua zana bora za kivita pamoja na kuwalipa wanajeshi wake mishahara minono.
Wakati ni sasa viongozi wa DRC kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya nchi yao kwani wakicheza watapoteza nchi yote.