Tetesi: DRC yaanzisha kikosi cha kijeshi kulinda migodi ya madini

JaxenDL

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2022
Posts
1,118
Reaction score
2,581

​

​

Mmoja wa maofisa hao alisema hilo ni wazo la Rais Félix Tshisekedi lenye lengo la kuleta mageuzi katika sekta ya madini na kupambana na ubadhirifu wa madini ya thamani.

Mamlaka ya madini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo imezindua kikosi cha wanamgambo kitakachohusika na kulinda migodi, kutekeleza sheria zake na kufuatilia kwa ukaribu uzalishaji wa madini.

Rafael Kabengele, mkuu wa shirika la madini, amesema kikosi hicho ni wazo la Rais Félix Tshisekedi kama sehemu ya mageuzi ya sekta hiyo na mapambano dhidi ya usimamizi mbovu wa madini ya thamani.

Awamu ya kwanza ya kikosi hicho cha kijeshi itakuwa na wanajeshi kati ya 2,500 na 3,000 ambao wanatarajiwa kuanza kazi Desemba 2026 baada ya mafunzo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili, lakini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za kuhakikisha wananchi wananufaika nazo.

Kufikia mwaka 2028, inatarajiwa kuwa watu 20,000 watakuwa wameajiriwa katika kikosi hicho kusimamia hadi migodi 22 katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Baadhi ya migodi, kama Rubaya mojawapo ya migodi mikubwa zaidi ya koltani duniani kwa sasa iko chini ya udhibiti wa muungano wa AFC M23.
Kikosi hicho kipya cha dola milioni 100, kinachoitwa Walinzi wa Migodi, kitachukua nafasi ya wanajeshi wa kawaida waliokuwa wakilinda migodi, na kimefadhiliwa na Marekani na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Wanachama wake watasimamia uchimbaji na usafirishaji wa madini ya thamani hadi yanapotoka nchini.
Inakadiriwa kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ina utajiri wa madini usiotumika wenye thamani ya dola trilioni 25, lakini sehemu kubwa ya wananchi wake bado wanaishi katika umaskini mkubwa na vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi.
 
Mhh...badala ya kuwa na jeshi imara la kulinda nchi yeye ameona awe na kikosi cha kulinda madini.
 
DRC watoe contract IRGC ili walindwe. Gharama itakua nafuu ila pia hata USA akitaka kugusa rasilimali zake anagongwa tu
 
vijana wa ki kongo wapo busy kujipamba na kuchubua ngozi waonekane weupe kama wanawake, na ajira zao ni kunengua viuno kwenye ma bar watalinda nini hao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…