#COVID19 DRC Yapokea dozi 250,000 za chanjo ya Moderna

#COVID19 DRC Yapokea dozi 250,000 za chanjo ya Moderna

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo imepokeadozi250,000 za chanjo ya Corona aina yaModerna.

Ni mara ya kwanza DRC kupokea chanjo nyingine isioyokuwa ya AstraZeneca.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi mwenyewe alisita kuchukua cha ya AZ na kuahidi kupewa chanjo tofauti wakati zitakapopatikana nchini.

Kundi hili la kwanza la dozi 250,000 za chanjo ya Moderna ni sehemu ya chanjo milioni sita tofauti ambazo Nchi hiyo ya Afrika ya Kati imekuwa ikingojea tangu, Julai iliyopita.

DRC ni moja ya nchi ambazo kuna pingamizi ya juu kupokea chanjo ya Corona barani.

Tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya chanjo dhidi ya covid-19, mnamo Aprili 19, 2021, chini ya watu laki moja wamepokea chanjo hizo. Zaidi ya dozi elfu 300 za AZ zililazimika kuharibiwa wakati zilipomalizika muda wa matumizi Juni na Julai iliyopita
 
Huku Afrika watu ni kama wametosa kupata chanjo...
 
Yani kwamba hata sisi afadhali au sijaelewa?
 
Back
Top Bottom