DRC yatangaza tena maambukizi mapya ya Ebola

DRC yatangaza tena maambukizi mapya ya Ebola

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola katika jimbo la Kivu Kaskazini hapo siku ya Jumapili baada ya mwanamke mmoja kufariki kwa ugonjwa huo, ikiwa ni miezi mitatu tu tangu mamlaka ya afya kutangaza kuwa mlipuko wa awali wa ugonjwa huo ulikuwa umedhibitiwa.

Waziri wa Afya, Eteni Longondo amekiambia kituo cha televisheni cha taifa, RTNC kuwa mgonjwa aliyefariki alikuwa mkulima, mjane wa mgonjwa aliyefariki kwa ugonjwa huo, ambaye alianza kuonesha dalili za ugonjwa huo Februari 1. Alifariki siku mbili baadaye, baada ya sampuli ya damu yake kuonesha kuwa na virusi vya Ebola.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilitangaza kumalizika kwa maambukizi ya 11 ya Ebola Novemba 18, 2020 ambayo yaligharimu maisha ya watu 55 kati ya visa 130 vilivyoripotiwa katika jimbo la Equateur pekee. Kusambazwa kwa chanjo kwa watu zaidi ya 40,000 kumesaidia kupunguza madhara ya ugonjwa huo.

Kurejea kwa Ebola katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo kunatoa changamoto mpya ya kukabiliana na mlipuko huo ambapo ufikiwaji wa raia unatatizwa na mapigano ya makundi yenye silaha na wanajeshi wa serikali. Mlipuko uliomalizika wa Ebola katika eneo la Kaskazini Mashariki uliodumu kwa miaka miwili ulikuwa mbaya zaidi katika historia ya nchi hiyo, ukisababisha vifo vya watu 2,277.

Mlipuko wa virusi vya ebola unaongeza chumvi kwenye kidonda, sasa DRC inapambana tena na milipuko miwili, ikiwa pia na visa 22,322 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 665.
 
Hivi huu ugonjwa mbona umewang'ang'ania wakongo kama kiroboto???
Hauwezi kuisha ili wazungu wapate upenyo wa kuiba mali iliyopo kongo vizuri.Ikishuka midege ya misaada kuondoka inaondoka na shehena ya madini.
 
Hatari sana , yaani huku waasi wa msituni + corona + ebola + serikali inayumba yumba = Mungu awasaidie tu maana hamna jinsi hapo
 
Back
Top Bottom