Rwanda sasa imepata uwezo wa kutoa huduma za anga ya juu kwa ndege katika anga lake pia kutoa huduma kwa ndege zinazokatiza anga lake
Mapigano ya M23 na serikali ya Congo, kuongeza gharama za uendeshaji wa RwandAir shirika la ndege la nchi ya Rwanda baada ya DR Congo kupiga marufuku shirika la ndege la Rwanda kutumia anga la Congo hivyo kuleta uwanja mwingine wa mapambano ya kiuchumi :
Mapambano yahamia angani : Kupanda kwa Gharama za Mchepuko wa miruko ya RwandAir Kutokana na Marufuku ya Anga ya DRC
Rwanda Air
FRI 14 FEB, 2025 16:40
Na
Bridget Nsimenta
RwandAir inakabiliwa na changamoto zinazoongezeka na kupanda kwa gharama kutokana na marufuku ya anga ya DR Congo, pamoja na muda mrefu wa safari za ndege, gharama kubwa za mafuta na kazi, na athari zinazoweza kujitokeza kwa uaminifu na faida kwa abiria.
Kufungwa hivi karibuni kwa anga ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ndege zilizosajiliwa Rwanda kumesababisha athari mbaya, sio tu katika mvutano wa kidiplomasia lakini pia katika changamoto kubwa za biashara kwa shirika la ndege la RwandAir.
RwandAir kubadili njia za ndege, ikiwa ni pamoja na njia yake kuu ya kuelekea Ulaya na miruko kuelekea Afrika ya Magharibi.
Siku ya Jumanne, Agence Congolaise de Presse iliripoti, ikinukuu mamlaka ya viwanja vya ndege ya Kongo, kwamba barua ya ndani ilitolewa inayopiga marufuku "kuruka juu na kutua katika eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa nchini Rwanda au zile zilizosajiliwa kwingineko nchini Rwanda kutokana na ukosefu wa usalama uliosababishwa na mzozo wa kivita."
Ingawa hatua hiyo inaweza kuonekana kama ujanja wa kisiasa, matokeo yake ya vitendo ni makubwa kwa shirika la ndege na abiria wake.
Ndege ya RwandAir ya Kigali hadi London, ambayo zamani ilikuwa njia ya moja kwa moja kupitia anga ya DR Congo, sasa inakumbana na mchepuko wa hadi saa mbili.
Abiria wameonyesha kufadhaika huku wengine wakifananisha uzoefu wao wa story za kutekwa nyara ndege. shirika la ndege la Ethiopia Airlines , likiruka juu ya anga ya DR Congo Alhamisi jioni, yalikuwa na hali ya wasiwasi katikati ya angani huku udhibiti wa usafiri wa anga ukithibitisha hali yao baada ya kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali.
"Ninahisi kama mmoja wa wale mateka wa bahati mbaya wa Palestina na Israeli katika vita vya Mashariki ya Kati ambavyo hawakuisababisha," Dk Sam Akaki, mmoja wa abiria wengi walioathiriwa alinukuliwa.
RwandAir imesema inatafuta njia mbadala ili kupunguza athari kwa abiria. Hata hivyo, Fiona Mbabazi, meneja wa masuala ya uendeshaji wa shirika hilo la ndege, hakujibu maswali Ijumaa kuhusu iwapo suluhu lilikuwa limepatikana.
Mchepuko huo wa miruko (flight path) sio tu huongeza matumizi ya mafuta lakini pia huongeza gharama za wafanyikazi kwa sababu ya muda mrefu wa mruko wa ndege.
Ripoti zimeibuka kuhusu baadhi ya abiria kutafuta mashirika mbadala ya ndege, lakini mtaalamu wa masuala ya anga mjini Kampala anaamini kuwa kuna sababu ndogo ya kuacha kuwa mteja mwaminifu (loyal customer).
"Kughairi kunaweza kusiwe chaguo kwa watu wanaosafiri kwa ndege ya RwandAir-wanaiona kuwa ina ushindani wa bei nafuu na wamezoea shida," mtaalamu huyo alisema.
Mtaalam huyo alipuuza wasiwasi kwamba mchepuko wa ziada wa saa mbili ungezuia abiria, akielezea kwamba upotevu wa muda unaweza kupunguzwa kwa ndege kuongeza spidi ya kasi.
"Kila shirika la ndege lazima litumie eneo lao lililotengwa maalum katika uwanja wa ndege ," aliongeza.
Gharama ya kubadilisha njia ya ndege kama Airbus A330, ambayo kwa kawaida hutumiwa na RwandAir kwa safari za masafa marefu, inakadiriwa kuongeza mafuta ya dola za kimarekani $72,354 kila siku.
Zaidi ya hayo, shirika la ndege hulipa gharama ya ziada ya U$67,586 kila siku, kutokana na kuongezeka kwa saa za safari za ndege na muda mrefu wa majukumu ya wafanyakazi.
Athari kubwa ni juu ya matumizi ya mafuta, ambayo ni ya juu wakati wa kuruka kwa kasi ili kupunguza upotevu wa muda.
Hivi sasa, safari za ndege kuelekea Afrika ya kati na Magharibi na Ulaya zinapitia Uganda na Sudan Kusini, kabla ya kuingia anga ya Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.
Wataalamu wanasema marufuku ya anga ya DR Congo sio tu suala la moja kwa moja kwa ndege zilizosajiliwa Rwanda; inaathiri mashirika mengine ya ndege pia.
Kwa kujibu uamuzi wa Kinshasa, pia Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uingereza ilitoa Notisi kwa Wanahewa, inayohitaji safari za ndege kukaa angalau maili 200 za nautical kutoka urefu wote wa mpaka wa DR Congo-Rwanda-Uganda pia iruke urefu wa angalau futi 25,000 ili kuepusha kupigwa kombora kwa bahati mbaya.
"Kwa hivyo kimsingi, ndege zote zitabidi kurekebisha miruko yao iwe mbali kabisa na kuambaa karibu ya mipaka ya Congo ," mtaalam alisema.
Utata wa uelekezaji upya huu unachangiwa na saizi kubwa ya anga ya DR Congo. Eneo hilo, ambalo lina ukubwa wa takriban nchi tano za anga za kitaifa, hutumika kama njia muhimu kwa mashirika ya ndege ya Afrika Mashariki kuruka hadi Ulaya.
Bila hivyo, mashirika ya ndege kama RwandAir yanalazimika kuruka umbali mrefu zaidi, na kuathiri faida na upangaji ratiba.
Mbali na kuongezeka kwa gharama, shida ya vifaa kwenye shirika la ndege ni kubwa. Safari za ndege za RwandAir kuelekea London hivi majuzi zililazimika kusimama kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda.
Kituo hicho ambacho hakikupangwa kiliongeza muda wa saa tano kwa ndege hiyo, na kusababisha abiria kufika saa nane na nusu kuliko ilivyopangwa.
Ucheleweshaji huo uliwaacha abiria wakiwa wamechoka, huku wengine wakionyesha kufadhaika kwa muda mrefu wa kusubiri, na muda mrefu zaidi wa majukumu ya wafanyakazi.
Wataalamu wa masuala ya usafiri wa anga wanaonya kuwa gharama za uendeshaji zilizoongezwa zinazohusiana na kukwepa kupita anga la DR Congo sio tu zitaathiri fedha za RwandAir lakini pia zinaweza kuathiri mauzo ya tikiti.
Abiria, ambao tayari wanakabiliwa na muda mrefu wa safari za ndege na bei za juu za tikiti kwa sababu ya maelekezo mapya, wanaweza kufikiria upya mipango yao ya safari, haswa njia mbadala zinapoibuka.
Muda ulioongezwa wa safari za ndege unaweza kusababisha wengi kutafuta safari za ndege zenye njia za moja kwa moja, iwe kupitia mashirika mengine ya ndege au ndege zinazounganisha ambazo zinakwepa anga ya DR Congo.
Usumbufu unaoendelea unatishia njia za Ulaya za RwandAir, ambazo ni muhimu kwa faida ya shirika la ndege, hasa kwa wasafiri wa biashara ambao wanategemea safari za ndege kwa wakati na za moja kwa moja.
Kufungwa kwa anga kuna athari kubwa zaidi, kuathiri huduma za RwandAir kwa Afrika ya Kati na Magharibi. Njia hizi, muhimu kwa muunganisho wa kikanda, pia zimetatizwa kwa kiasi kikubwa, na kulazimisha shirika la ndege kubadilisha njia hizi za ndege na kuongeza zaidi utata wa uendeshaji.
Changamoto ya RwandAir inakumbusha uzoefu wa Qatar Airways wakati wa kizuizi cha kisiasa cha 2017. Qatar Airways, iliyopigwa marufuku kuruka katika anga ya nchi kadhaa jirani, ililazimika kuchukua njia ndefu na za gharama kubwa zaidi.
Shirika hilo la ndege, ambalo linafanya kazi pekee katika njia za kimataifa, lilikabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha kwa miaka mingi, likichapisha hasara mfululizo kutokana na kizuizi hicho.
Kama vile RwandAir, Shirika la Ndege la Qatar lilikabiliwa na gharama ya juu ya mafuta, kuongezeka kwa changamoto za uendeshaji, na matatizo ya kuridhika kwa abiria kutokana na kuchelewa na kubadilishwa kwa njia za ndege.
Hali ya Qatar Airways ilizidishwa na mapungufu ya uwezo wa kubadili njia za mruko na athari za janga hilo. Walakini, kizuizi kilipoondolewa mnamo 2021, shirika la ndege lilipata tena njia zake bora za ndege, na kuongeza mapato na kurudi kwenye faida.
RwandAir inaweza kupata afueni sawa pindi hali ya kisiasa na DR Congo itakapotatuliwa, na kuiruhusu kurejea kwenye njia za ndege za moja kwa moja na za gharama nafuu.
Madhara mapana ya marufuku ya anga ya DR Congo yanahusu, sio tu kwa RwandAir lakini kwa sekta ya anga ya kikanda kwa ujumla.
Kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kunaweza kusababisha bei ya juu ya tikiti, na kufanya njia za Afrika Mashariki kutokuwa na ushindani ikilinganishwa na safari zingine za ndege za kimataifa.
Zaidi ya hayo, kutokuwa na uhakika kuhusu sera ya anga ya DR Congo kunaweza kuzuia wawekezaji watarajiwa katika RwandAir, na kuzuia matarajio ya ukuaji wa shirika hilo.
Wataalamu wanaeleza kuwa kufungwa kwa ghafla kwa anga huvuruga sio tu mashirika ya ndege bali pia usafiri wa anga duniani kote, jambo linaloibua wasiwasi kuhusu usalama na ufanisi wa uendeshaji.
Shirikisho la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) wamesisitiza kwamba kufungwa kwa anga kunapaswa kushughulikiwa kidiplomasia, na miundo imewekwa ili kupunguza athari mbaya kwa trafiki ya anga ulimwenguni.
Kwa sasa, abiria wanaosafiri kwa ndege kutoka Kigali hadi London na maeneo mengine ya Ulaya lazima wakabiliane na muda mrefu wa ndege, ucheleweshaji unaowezekana na gharama kubwa zaidi.
RwandAir inaendelea kutafuta njia mbadala zinazofaa, lakini ushuru wa kifedha (kodi) na kiutendaji unasalia kuwa mkubwa.
Kama Qatar Airways, inaweza kuchukua miaka kabla ya matokeo kamili ya kifedha ya marufuku ya anga kueleweka, inategemewa RwandAir itakumbana na changamoto kama za Qatar Airways.