Dreamliner imejaa wiki nzima! Hongera ATCL na pongezi kwa Rais Magufuli, unaona mbali

Bandiko muruaaa kabisa. Ila hapo kwenye headsets naungana na ATCL kamwe wasithubutu kuweka. Sisi wabongo hatuna ustarabu hata chembe. Zikiwekwa tu hatukawii kushuka nazo aisee.
 
Amefanya kitu gani alichoahidi kwenye hotuba ya bungeni?
- Ujenzi wa reli mpya ya kisasa na kufufua reli ya Tanga.
- Kufufua shirka la ndege lililokuwa na ndege moja na sasa lina ndege 7
- Kuimarisha ufanisi katika huduma za bandari.
- Kuongeza huduma za maji (Juzi tu Mh Mbarawa amepewa zaidi ya trilioni moja kufanikisha hilo)
- Ujenzi wa bwawa la umeme mto rufiji (maandalizi yamesha anza)
- Kuongeza ufanisi wa kazi serikalini'
- Kuongeza huduma za afya na kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana nchini.
- Kupitisha sheria mpya ya maliasili.
- Kubana matumisi yasiyo na tija kama Kupunguza safari za nje kwa viongozi wa serikali.
- Kudhibiti miaya ya wizi na kuongeza ukusanyaji wa kodi.
Nakadhalika...
 
Pongezi upo sahihi kabisa Mkuu ila Mara Mimi msukuma sijui mnyamwezi kwenye nyuzi muhimu ukabila wa nini sasa punguza ukabila hausadii kitu chochote katika maisha yako...Mwalimu alipinga sana kutambuana kwa makabila bado mliokuepo akipinga kitu muhimu mnakitumia ili iweje...
 
wachumi huwa tunaangalia biashara inaendeshwa kwa faida au hasara ?
ungebandika bandiko la gharama za uendeshaji na faida..
si uzuri wa chombo, uzuri wa wahudumu na kujaza au kutojaza..
ni mapema mno kuzungumzia mafanikio ya dreamliner
wachumi tunajua huhitaji miaka kadhaa maana kurudisha tu gharama si mwaka leo wala mwaka kesho..
PAMBANA BROO UNAWEZA KUUKWAA KAMA GONDWE
 
IATA - Current Airline Members
 
Mkuu hukuwa kupata namba ya simu ya angalau binti mmoja mhudumu wa hiyo Dreamliner? Maana umenishawishi kwa kuwasifia
 
China wasafiri wengi watakuwa Wachina, Kilimanjaro watakuwa wachaga na Mwanza wasukuma na Wanyamwezi wote wanajua Kiswahili. Lakini Kwenda India ni Kihindi. All languages are important and useful.
 
ATCL kazeni buti, hatua ni nzuri, weken target ya kila mwaka mnaongeza ndege moja, msibweteke eti mna ndege sita bado hazitoshi kutoa huduma katika nchi nyingi, tunataka shirika imara linalo toa huduma bora na lina linakwenda sehemu mbalimbali duniani, achaneni na siasa, siasa katika nchi hii ni nyingi ndio maana tuko hapa.
 
Lile dude ikifika zam yake kuboard lounge huwa inabaki nyeupe, ila kabla huwa hata viti vya kukaa hamna, pia ac huwa zimezidiwa nimeshalipanda maramoja, observation zako zipo sahihi, ila kwa safari ya lisaa moja haina maana ya headphones
 
Air Tanzania.Iendelee kujipanua lakin tuhakikishe weledi utawale kwa kila sekta ya uendeshaji.Ujanja ujanja tuweke pembeni. Tuzidi kumwombea rais wetu aendelee kupata maono kama haya bila kukurupuka.
 
Wasukuma wakiwa na hela hawana ubahiri kama wapare au wakinga. Wao huwa wanakuwa kama wakongo. Full kujiachia
 
Daah sifa zingine za kijinga kwaio ndege kijaza watu anasifiwa Raisi? Kwani yeye ndo muuza tiketi na mtoa matangazo? Au mfanya booking? Hivi vitu mbona havikuwepo enzi za JK mambo kama kuanza kusifia vitu vidogo vidogo no dalili na ishara kwamba watu hawana hoja za msingi bali ni kujilamba lamba
 
Jitahid bro upate sub half time ndo iyoo inakarbia kukata kipindi cha atun uhakika nacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…