Dreamliner imejaa wiki nzima! Hongera ATCL na pongezi kwa Rais Magufuli, unaona mbali

Mwamba,Wabeja sana.Hizo Bombardier CS300 tuliambiwa zinaingia mwezi Novemba 2018 usijali mambo yataendelea kuwa bam bam chini ya Uongozi wa Mhe.Magufuli.Kwa ujumla jiji la Mwanza lina biashara nzuri ya ndege kwani hata makampuni mengine yanapeleka ndege 2 hadi 3 kwa siku na zinajaa.Ila ATC mbarikiwe sana kuna Kampuni Fulani ya ndege ilikuwa inatunyanyasa sana abiria e.g kutuuzia refreshments kwenye ndege,kilo za mizigo hususan ndoo za SATO wa Mwanza nk. ilikuwa shida tupu.Sasa hivi wameamua kulegea.Go go ATC the wings of Kilimanjaro!
 

Paschal...nimelipenda andiko lako ni zuri..ila sikupendezwa na jambo moja: kutaja taja 'wasukuma'...ushauri wangu ni kuwa jiepushe na hii tabia ya kutaja taja makabila...najua umeandika kwa nia nzuri tu na kwa utani...lakini mambo siku hizi yamebadilika...wako ambao wana elements za ukabila...na wanachukulia kutaja taja makabila kuwa ni agenda yao....watanzania hatuna ukabila na hili tunashukuru kwa jitihada za viongozi wetu waasisi wa taifa hili na hasa Mwalimu Nyerere....lakini watu wengi na hasa vijana wengi hawajui kuwa inawezekaana pengine in Africa ni Tanzania pekee isiyo na ukabila...sasa mitandao au sociaal media ni nzuri lakini zina ubaya wake ..zinaweza kutumika pia kuleta mabaya yakiwemo ya ukabila...tusije taje makabila humu sijui wasukuma, wagogo wachaga na kadhalika....tunadike tu watanzania wanajaza ndege na siyo sijui wasukuma, wachaga na kadhalika...
 
Naam! Dreamliner inatakiwa iwe hewani kwa zaidi ya masaa 4000 kwa mwaka (ikiwa unakaa abiria) to break even. Sidhani kama safari za ndani zitatosha kufikisha masaa hayo. Kwanza, Itahitaji kuwa na safari za nje, kwa mfano Dar - Guangzhou (china), Dar - Bombay, Dar - Ankara through Dubai. Pili, tujiulize kama kuna connection toka Dar kwenda nchi zingine zikiwemo za kwenda West Africa, ili abiria wa nchi hizo wapande ndege yetu. Tatu, wasafiri kwenye hizo route ni wafanyabiashara wanaobeba mizigo zaidi ya kawaida. Sijui kama configuration ya ndege hiyo imebeba hilo hitaji. Nne, route hizo pamoja na kuweka hizo connections toka Dar zinahitaji kuwepo na angalau dreamliner mbili au zaidi. Tano, wadhibiti wizi! Mengine yatategemea umahiri wa ATCL kujiuza! Biashara hii ni ngumu sana, mashirika mengi yanapata hasara: fastjet, South African, .... na hii inasababishwa na Serikali kuingilia hii biashara na kutaka nchi iwe na ndege. Hii ni vyema ikaachiwa watu binafsi.
Kila la kheri, tumeshajitumbukiza humo, wapigane kupata faida! Wasirudi na bakuli baadaye kuomba msaada hazina!
 
Paskali usiogope kuonekana na hawa wapinzani wetu uchwara unaunga mkono jpm moja kwa moja kwa sababu jpm ni wakuunga mkono sana. Huyu ni economic visionary leader ila yeye ni mass leader sio wa class ya kibwanyenye. Hapo sasa ndio kuna ugomvi na vibepari uchwara na wa nje wenye ubinafsi..sioni shida kama una fedha kwa nini ukope ndege au ukodishe. Ni marketing influence tu ya mabenki na watu wa kati. Kwani ukikopa unakopa bure si lazima kuna interest? Tena kukodi ndio balaa maana watu wetu wanaweka cha juu hata mtu hajaenda shule anaona gharama kubwa kwa kipindi kifupu kuliko kununua ndege yako mpya. Atc kabla wamekua wanakodisha ndege umeona faida gani kama sio hujuma na wizi wa wakurugenzi na mameneja. Imekua kichochoro cha wizi na hujuma wa fedha za umma kwa muda mrefu hadi jpm kuvunja hicho kijiwe cha wezi.
 
Naunga mkono hoja. Mwanza siko pa kupeleka vindege vidogo vidogo, huko zinahitajika jet za maana tu.
 
Dreamliner kwa local root?? kaka hata uwajaze wasukuma hadi kwenye carrier huwezi pata faida!! Pongezi za nini hapa!!

Unashabikia under-utilization ya resorces za umma??
 
Tanzania kati ya route potential zinazolipa ni Mwanza-Dar, hapa hakuna upendeleo!
 
Namba 7,8 na10 wafanyie kazi haraka sana maana soon hilo dege litaanza kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu,wasituangushe tafadhali...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…