Dreamliner imejaa wiki nzima! Hongera ATCL na pongezi kwa Rais Magufuli, unaona mbali

Mkuu kaka Pascal, nakuheshimu sana humu; well, nimepanda ndege hi mara 2 na hata zile zingine za aina ya bombadia na zenyewe nimepanda mara 2, hi unayo izungumzia hapa ni kweli ya kisasa sana na ni nzuri na ni kweli kwamba unavyo taka kuanza ku enjoy tu, mara mnatangaziwa "prepare to land". Hao abiria wengi wa Mwanza unao wasifia sio wote WASUKUMA kaka, mimi na wanangu ni miongoni mwao, nimekwenda sana Mwanza na hi kitu (hili sio muhimu, just joke)
Kitu kingine ambacho ningependa na mimi kupendekeza ni ile route ya Mwanza-KIA, kwanini waliiondoa!? Precision naona kaweka bei za kukomoa hasa, route moja inakwenda hadi laki 4 from Mwanza to Moshi? Sio fair kabisa, mwezi Augost nimepanda hi ndege from Mwanza to Dar and then pia nilipanda from Mwanza to Moshi only for Tsh 93000 pamoja na kodi, was very nice trip. Well done Magufuli on this but kingine ambacho nina hakika kaka mkubwa umekisahau ni hiki, mkuu angeimarisha institutions kama anavyo shauriwa na wengine, tukumbuke hili shirika la ATC sio jipya, lilikuwepo tokea Enzi za mwalimu JK Nyerere, wengine walivyo kuja ndio hivyo tena, wakalipeleka ICU, mhe Magufuli akitoka madarakani, ATCL itaendelea kua hewani!? Something to think about.
 

Akili za watu wajinga hupelekea kiama ktk nchi yao, zama za sasa za uongozi ktk taifa letu ni janga,biashara syo ndoto unaamka unaanza kuifanya, ujinga ndo ulotumika kununua ndege bila mhimili wa bunge kuhusishwa,hakuna wataalamu waliohusishwa zaidi ya jiwe na mjomba mtu.
Hatuwezi kamwe kufurukuta ktk nyanja hii ya usafiri wa anga.wenzetu kenya bado wanasuasua, rwanda na hata s/africa sembuse chato
 
Jumamosi iliyopita haikuja Mwanza, nisikilizie tulivyokuwa tunaondoka kwa mafungu. Niliondoka na ndege ya saa saba usiku (Bombardier) na kufika Dar saa 9 usiku. Pia premises za Mwanza hasa boarding area imeshakuwa ndogo sana kwa influx ya wateja wa ndege zote, ATC, Fast Jet na Precision.
 
Karne ya 21 unapanda ndege ya ukabila? Sisi waha na wajomba zangu wahaya tusemeje? Aibu hii
 
Ndugu yangu Pascal, kwanza nipende kukupa pongezi za dhati kwa uzi huu. Nimekusoma na kukupata haswaa. Pamoja na pongezi nimejikuta ninakaswali (out of curiosity). Hakuna ubishi kuwa Mkoa wa Mwanza ni kituo kikuu cha usafiri wa Anga kwa Kanda ya ziwa, inayoundwa na mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara na Shinyanga (sina uhakika). Kwa msingi huo ni bayana basi kuwa Watu wa mikoa yote hiyo wanatumia usafiri huo wa dreamliner. Sasa wewe umewezaje kujua, miongoni mwa abiria wa kanda hiyo, kuwa Wasukuma ndio wanaoongoza kupanda ndege; na sio Wahaya, au Watu wa Mara?



Lakini nipende pia kusema umeniacha mdomo wazi kwa sentensi yako hii “Jana mimi mwenyewe ilinilazimu kutumia ile sayansi yetu ya asili, kumfanya abiria mmoja awe no show, ili niweze kusafiri”. Imani yangu ni kwamba sentensi hii imekuja kwa lengo la kunogesha uzii. Kama sivyo naomba uieleze Dunia kwa mapana juu ya hiyo sayansi, maana yaelekea mwenzetu unaifahamu.

Ni hayo tuu kwa sasa
 
Yani unapoanza na ukabila unatufedhehesha Wasukuma tunaotumia akili.

Pia unapotoa pongezi kwa Dreamliner, dege la masafa marefu, kupaa Dar to Mwanza, naona huna standards za kuona tulitakiwa kuwa kama Kenya wenzetu jana wamerusha ndege moja kwa moja Nairobi mpaka New York.

Yani badala ya kupitia Amsterdam au Zurich tutakuwa tunakuja Bongo kwa kupitia Nairobi. Unakula Breakfast New York, dinner Nairobi.

Hayo ndiyo mambo tunataka kusikia.

ATC Dreamliner ilikuwa hata haiwezi kuruka nje kwa sababu hatukuwa na uanachama IATA. Ndiyo kwanza tumeurudisha.

Sikulaumu sana.

Una low standards.
 
Pongezi za dhati kwa Rais wetu mzalendo wa kweli na serikali anayoiongoza,baraka za Mungu zisiwapungukie.
 
kumbuka watu wa bukoba hupitia mwanza na ndege zinaishia bukoba
 
I like it unasoma ukienjoy
 
Mkuu mimi nimekuelewa! Umetumia lugha ya picha sana! Umesifia weeee,umemsifia jiwe weee ukaingizia na usukuma basi hapo jiwe kafurahi sanaaa! Halafu mwishoni umekuja kimchana ukweli mchungu,heheheh! Haya siku njema! Next episode atununullie Terrible teens,dreamliner zishachuja
 
Paskali, sikupingi na pongezi zako, ila kujaza ndege ni moja na kuiendesha kwa faida ni jambo jingine. Dreamliner ni ndege ya masafa marefu hivyo inavyotumika kwa masafa mafupi ni aghali zaidi. Hizi safari fupi za mwanza - dar zingefaa zifanywe na Boeing 737 ndipo ingekua faida.
 
FAO LA KUJITOA

Hao wanyonge wanaotetewa ni akina nani?

Au Lazima nchi iwe na wanyonge milele ili wasaka tonge wapate umaarufu

Mara huku DEGE eco village kigamboni, mara kule majengo hayana wapangaji?

ili mradi tu wametafuna pesa za wanyonge...Kwel laana hii itawapata kuanzia watoto mpaka wajukuu, wallahi
 
Kwa vile zilitolewa hoja humu kuwa Dreamliner haijai, nimepanda na nimeshuhudia imejaa full, kwa hili tuu ATCL inastahili pongezi, ila pia pongezi ziende pia kwa aliyenunua ndege hizi
Mkuu Paschal naungana na wewe kutoa pongezi.
ila nakuomba usifurahie ndege kujaa bali nenda hatua moja
mbele ya kujiuliza je,hao wanaojaza ndege wanalipa nauli?
isije ikawa ni ndugu wa watumishi wa ATCL au maafisa
waserikali,ukachekwa.Yesu aliwaambia wanafunzi wake
kuwa "Msifurahi kuona mapepo wamewatii,bali furahini
kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni".
 
Wenye maupepo yenu@ tiss
 
Eng.Matinde ni kabila gani vile? Hao abiria wametoka wapi ghafla? Mbona enzi za Bombardier na fast jet zilikuwa hazijai? there is something fishy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…