Kweli Caren, nategemea kutumia Drop Irrigation System katika mradi wangu wa kilimo cha mapapai, ambapo nategemea kutengeneza mwenye (local); nimeuliza katika duka moja hapa dodoma la vifaa vya kilimo wana hizo pipe kwa ajili ya drop irrigation; hivyo basi nitanunua tank la lita 1000 na kuunganisha mwenyewe hizi pipe kwenye kila mstari wa mche na kutoboa tundu dogo katika kila mche. Nitaweka katika post yangu hatua zote nitakapofikia, hivyo usisite kuniwezesha katika mradi wangu. Nafikiri kwa kuanza na kama ni mradi mdogo, basi unaweza kujifunza system yenyewe ilivyo na kujaribu ku-implement kwa kutumia vifaa vya kawaida; kwani huko kwenye mashamba ya maua wanatumia vifaa vya kisasa zaidi ambapo vingarimu sana, nilishawahi kuhuduria maonyesho ya vifaa vya kisasa kwa drop irrigation kwa kampuni moja kutoka Israel, kwa kweli ni gharama sana; inahitaji mradi mkubwa sana.