DROGBA KUJENGA HOSPiTALI TANO kwa ajili ya wanawakena watoto, IVORY COAST

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
KUPITIA taasisi yake ya kutoa misaada, nahodha wa Ivory Coast na gwiji wa Chelsea Didier Drogba atasaidia ujenzi wa kliniki tano za watoto na wanawake katika nchi yake. Tangazo hilo lilitolewa na katibu mkuu wa Didier Drogba Foundation Guy Roland Tanoh, ambaye alisema kwamba ujenzi wa kliniki hizo utafadhiliwa na Taasisi ya London galas pamoja na fedha Drogba mwenyewe. (HM) Tanoh amesema kiasi cha 2.5 billion CFA francs ($5 million)
kitatumika kuwekeza katika ujenzi wa kliniki hizo, huku
zikijengwa katika miji mitano mikubwa ya nchi hiyo Abidjan,
Yamoussoukro, Man, Korhogo na San Pedro. “Drogba aliendesha mchango huko London na zikapatikana
kiasi cha $ 2 billion CFA francs ($4 million),” Tanoh alisema.
“Kiasi kilichobakia cha million francs ($1 million) hakitakuwa
tatizo kuona ndoto ya mwenyewe Drogba ya kuona afya za
wananchi wa Ivory Coast zinapewa kipaumbele.” Drogba mara ya kwanza alitangaza mpango wake wa kujenga
hospitali kubwa katika jiji la Abidjan mwaka 2009 akitumia fedha zote - kiasi cha £3 million ($4.5 million) alicholipwa na Pepsi. Lakini badala ya kujenga hosptali hiyo moja kubwa
akaamua ambayo ingekuwa mjini tu, akaamua kujenga vituo
vitano vya afya katika mikoa mingine ili kuweza kusambaza
vizuri huduma za afya. Chanzo: Supersport
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…