Drogba Vs Rooney: Katika Ubora Wao Ulimkubali Yupi?

Drogba Vs Rooney: Katika Ubora Wao Ulimkubali Yupi?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kwa nyakati fulani, hawa walikuwa mastraika tegemeo kwenye vilabu vyao. Didier Drogba "The African James Bond" akiwa tegemeo kubwa pale Chelsea ilhali Wayne Rooney "Wazza" a.k.a "The White Pele" akiwa muhimili wa mafanikio Man Utd.

Nyakati zimekimbia, Drogba ameshastaafu soka la ushindani wakati Rooney yupo akimalizia soka lake huko Marekani.

Kama uliwahi kuwashihudia mastaa hawa wakitamba EPL na UEFA, tuweke ushabiki wa vilabu vyetu kando, yupi ulimkubali sana?

IMG_20191114_143247.jpeg
IMG_20191114_143156.jpeg
 
WAYNE MARK ROONEY
Binafsi namkubali sana hadi leo, alikua anacheza kama mshambuliaji, kama kiungo, ana asist, anafunga, anapiga zile pasi za mtaa kwa mtaa, anakaba.

#Wazza #TheWhitePelle
Hahaha eti pasi za mtaa kwa mtaa. Nafikiri zile alikuwa akimuiga Paul Scholes. Wazza ni complete package. Hakuwa na kipaji kikubwa sana ila alikuwa ni mpambanaji wkwa asilimia 100. Kwakifupi ni mfia timu.
 
Didie drogba nilipenda cos alikuwa mchezaji kwa ajili ya mechi kubwa
A man for big occassion! Nani hakumbuki lile goli lake la kusawazisha dhidi ya Bayern Munich katika fainali ya UCL. Kisha dakika chache baadae akaenda kupiga penati ya ushindi, Chelsea wanatwaa ndoo!
 
Rooney ni habari nyingine mfumo mzima wa timu ulikuwa unamtegemea yeye ndio maana asipokuwepo karibia mfumo mzima wa timu unakuwa chini ya kiwango yaani kianzia katikati mpk kwenye ushambuliaji , kumbukumbu nzuri Uefa 2010 Bayern walimjeruhi kwa makusudi ili akose mechi ya marudiano akudungwa sindano ili awepo tu uwanjani kingine mjamaa hata kukaba anakaba sometimes anarudi kudifense na tackle anapiga fresh tu.
 
Kwa nyakati fulani, hawa walikuwa mastraika tegemeo kwenye vilabu vyao. Didier Drogba "The African James Bond" akiwa tegemeo kubwa pale Chelsea ilhali Wayne Rooney "Wazza" a.k.a "The White Pele" akiwa muhimili wa mafanikio Man Utd.

Nyakati zimekimbia, Drogba ameshastaafu soka la ushindani wakati Rooney yupo akimalizia soka lake huko Marekani.

Kama uliwahi kuwashihudia mastaa hawa wakitamba EPL na UEFA, tuweke ushabiki wa vilabu vyetu kando, yupi ulimkubali sana?

View attachment 1263016View attachment 1263017
Iko hivi, drogba angekuwa mzungu angepewa heshima yake n rooney angekuwa mwafrika tusingesikia lolote kuhusu yeye maana hata etoo kamzidi sana.
 
Iko hivi, drogba angekuwa mzungu angepewa heshima yake n rooney angekuwa mwafrika tusingesikia lolote kuhusu yeye maana hata etoo kamzidi sana.

Acha hizo mkuu, Pele Ni mweusi na alikuwa, vipi kuhusu Eusebio na Weah

Naomba nikuulize kati ya Eto na Drogba nani zaidi?

Wenzetu wana mifumo mazuri na watu wanaishi dream zao, Adebayor alisingizia kulogwa, ya Eboue unayafahamu pia?
 
Muulize mleta uzi kwa nini kaleta huu uzi! Kama alijua ni rooney basi haikuwa na haja ya kuweka uzi humu.
Hayo ni mawazo yangu.
 
Usimfananishe King Drogba na Rooney ..uyo uingereza ulim'beba...

Mpaka anafikia kuitwa King ..sio kazi ya kitoto ..

Live long Lengend Didier Drogba King...

Kila la kheri Chelsea[emoji170][emoji170][emoji170]
Hiv drogba Naye alikuwa mchezaji kumbe ????...
 
Back
Top Bottom