Drywall na ujenzi wa kisasa

“Wabongo tuache kuingiza iphones kutoka nje” hayo maneno yameandikwa na nani? Kama unatangaza biashara tangaza vizuri utapata wateja.
Naona umekusudia kuharibu huu uzi, hoja yako haina mashiko.

emekushika pabaya kwenye i phone.
 
Nyumba ya drywall tupu inajengwa hivi:

Halafu wanamalizia kwa kuweka siding. Hii nyumba tofali zipo kwenye msingi tu.

Hizi nyumba za USA tunazijua unafikiri unaweza kujenga Maramba mawili hio. Watakata hizo mbao mkuu. Huku wanakata grill au wanatoboa hadi ukuta wa tofali hizo mbao si watakufanya mtaji?
 
Hizi nyumba za USA tunazijua unafikiri unaweza kujenga Maramba mawili hio. Watakata hizo mbao mkuu. Huku wanakata grill au wanatoboa hadi ukuta wa tofali hizo mbao si watakufanya mtaji?

Pima faida na hasara yake. Halafu jiulize USA na Tanzania ni wapi wana vifaa vizuri vya kutobolea ukuta. Bila ya kusahau nyumba za Tanzania zina majirani na wapangaji. Hata jogoo wakiona songombingo wanaweza kupiga kelele[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pima faida na hasara yake. Halafu jiulize USA na Tanzania ni wapi wana vifaa vizuri vya kutobolea ukuta.
Wewe unafikiria nini? Wanaotoboa no vibaka. Unafikiri USA kuna vibaka wa kuja kuiba flatscreen au home theatre? Unafikiri kwanini bongo tuna grills madirishani na milangono wakati USA kuna milango tupu tena mingi ya plastiko na vioo?
 
Ni nzuri lakini hakuna siri hapo nyumbani. Sauti chumbani inasikika hadi barazani....sio sound proof......jipangeni mnao taka kutumia hizi
 
Wewe unafikiria nini? Wanaotoboa no vibaka. Unafikiri USA kuna vibaka wa kuja kuiba flatscreen au home theatre? Unafikiri kwanini bongo tuna grills madirishani na milangono wakati USA kuna milango tupu tena mingi ya plastiko na vioo?

Inategemea na eneo unaloishi. Hii ni Marekani.
 
Mabadiliko na maendeleo ya kweli hufanywa na wananchi sio serikali.

Tusijitishe wenyewe kwa kuogopa maendeleo. Kuna watanzania wengi hawajaona ujenzi huu. Wakijifunza hapa na kuelewa faida zake na wakaona ni ujenzi unaowafaa, huo ni mwanzo wa mabadiliko.
Na ndipo watakapofikiria jinsi ya kupambana na hao vibaka watakaovunja ukuta.
Kusema ukweli nyumba hizi ni salama. Kwanza ieleweke hakuna drywall inayowekwa kama ukuta wa nje. Hii ina maana mpaka kibaka akifika kwenye drywall ameshaingia ndani ya nyumba.

Na pia muda atakaotumia kukata mbao na drywall afadhali ang’oe mlango au dirisha.

Kuta za nje zinajengwa kwa tofali, vioo au siding. Kwa Marekani kwenye nyumba za makazi ya watu siku hizi wanatumia siding kwa nje ndani wanaweka drywall. Tofali za nje zinatumika kwa mapambo tu.
 
Matengenezo yake ni rahisi unaweza kuziba au kuweka kipande kingine cha drywall mwenyewe bila ya kutumia fundi.
Unajuanhizi ndoa za kibongo ugomvi ni kawaida sana, mke na mume wakisukumana kidogo tu litachanika lote hilo, vipi paa likivuja na kulilainisha kama boksi..
 
Unajuanhizi ndoa za kibongo ugomvi ni kawaida sana, mke na mume wakisukumana kidogo tu litachanika lote hilo, vipi paa likivuja na kulilainisha kama boksi..

Fujo za nyumbani ni kawaida popote pale duniani. Hizi kuta zinatumiwa na watu ambao kuvuta bangi ni ruksa kwa mujibu wa sheria.

Paa likivuja linaacha madoa tu kama ya kwenye silingi bodi. Likiloa kabisa unatoa na kuweka kipande kingine.
 
Hayo makitu ndiyo yanawekwa ndani ya drywall.
Hizo ni insulating materials ili kuhifadhi joto nyakati za summer or winter kunapowashwa aircon au heaters...

Sasa kwa 'bongo' ukijenga nyumba halafu yakawekwa hayo madude na nyumba isiwe na AC, wakati wa joto unaweza ukatamani kuvua ngozi...
 
Nyumba ya drywall tupu inajengwa hivi:

Halafu wanamalizia kwa kuweka siding. Hii nyumba tofali zipo kwenye msingi tu.

Msingi huwa ni concrete slab hakuna tofali hata kidogo
 
Hizo ni insulating materials ili kuhifadhi joto nyakati za summer or winter kunapowashwa aircon au heaters...

Sasa kwa 'bongo' ukijenga nyumba halafu yakawekwa hayo madude na nyumba isiwe na AC, wakati wa joto unaweza ukatamani kuvua ngozi...

Nyumba za Bongo hata AC hazihitaji. Zinahitaji madirisha ya kupitisha hewa. Wabongo hatujui jinsi tulivyojaliwa hali ya hewa nzuri.
 
WEKA HABARI KAMILI MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…