DSE:Taarifa za fedha kwa "listed companies" soko la hisa la Dsm ziwe kwenye Kiswahili.

article

Senior Member
Joined
Sep 10, 2016
Posts
186
Reaction score
344



Habari,

Taarifa za fedha hasa za robo ya mwaka na za mwaka kwenye makampuni yaliyosajiriwa DSE zimekuwa zikichapishwa kwenye lugha ya kiingereza na kushindwa kufikia malengo ya Taarifa za fedha kwa mujibu wa malengo ya Taarifa ya fedha kama vile 'IASB' inavyotaka.

Lengo kuu la Taarifa za fedha (Statement of comprehensive income,Statement of financial position (Balance sheet),Statement of cash flow, Statement of changes in equity na Notes to account) ni kuwawezesha wadau(wadau ni kama vile wamiriki wa hisa,serikali, wasimamizi,wateja, wafanyakazi wa kampuni husika,wadai na wadaiwa wa kampuni husika na umma kwa ujumla) kufanya maamuzi sahihi ya kiuchumi juu ya Taarifa hizo kama vile kununua au kuuza hisa za kampuni husika,kuendelea kushikilia hisa,kuendelea kufanya au kusitisha biashara na kampuni husika,kujua jinsi gani kampuni husika inavyotii kanuni au sheria zinazosimamia utekelezaji wa shughuli zake.

Kwa kuwa lugha inayotumika kufikisha taarifa kwa wadau wengi haileweki vizuri na wadau walio wengi wa DSE, uongozi wa DSE hauna budi kuzitaka kampuni zote zinazouza hisa hapo kuanza kuchapisha Taarifa zake za fedha kwa kiswahili hasa zile za robo (quarter) kwenye vyombo husika.Kiswahili ni Lugha ambayo inaeleweka karibia na wadau wote wa DSE ukilinganisha na kiingereza kinachoeleweka kwa wadau wachache.

Jambo ili litaongeza ufahamu wa wadau kuhusu usalama na uwekezaji wa mitaji yao na kuongeza uwazi katika utendaji wa kampuni hizi na kubwa zaidi ni kuwawezesha wadau kufanya maamuzi sahihi yanayohusiana na kampuni husika huku Taarifa za fedha zikiwa ndio msingi mkuu wa maamuzi yao.

Taarifa hizi pia zitolewa katika lugha ambayo inaeleweka katika lugha ya kawaida ya kiswahili kwa kuwa kumekuwa na visingizio visivyo na msingi kwamba ni vigumu kutafsri misingi ya uandaaji wa Taarifa za fedha nikimaanisha IASs na IFRSs.

Nimekuja na hoja hii baada ya kufanya utafiti na kugundua kwamba wadau wengi wanapata shida kufahamu kiundani taarifa za fedha hasa zile zinazoandaliwa kwenye lugha za kigeni hasa kiingereza na kuwapelekea kufanya maamuzi yasiyo na faida kwenye uwekezaji wa hisa na kuishia kupata hasara kubwa au manufaa yasiyoendana na mtaji wanaowekeza katika hisa kwa kukosa taarifa inayoeleweka juu ya uwekezaji wao wa mitaji.

Pia DSE wahakikishe taarifa za wakaguzi hawa zinatolewa katika lugha ya kiswahili pia hasa "KAM"(Key audit matters) ili kuboresha zaidi uelewekaji wa taarifa za Fedha zilizokaguliwa.

Nawakilisha,

Article.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…