Ninavyofahamu mimi Jiji la Dar, Madiwani wa Ukawa 53, CCM 38.
Jiji la Tanga, Madiwani wa Ukawa (CUF) wapo 16, CCM wana 11. Jiji la Arusha ndiyo funga kazi, Madiwani wa Ukawa(Chadema) wapo 24, CCM wameambulia diwani 1, Jiji la Mbeya Ukawa( Chadema) wana madiwani 18, CCM wana 6. Mji wa Moshi Ukawa (Chadema) wana madiwani 18 na CCM wameambulia 3, Mji wa Iringa Ukawa(Chadema) 14 na CCM wana madiwani 4.
Kwa hiyo ingawa CCM inatamba kuwa imeshinda, lakini kiuhalisia imeshinda 'maporini' na kwenye miji mikubwa na yenye uwezo mkubwa kiuchumi almost yote ipo chini ya Ukawa except Jiji la Mwanza ambalo ni home city kwao Magufuli.