DSTV yazindua kifurushi cha 17000, nafuu mno

km DSTV haina supersport 3 kwenye kifurushi chake hamna haja ya kununua...maana ni afadhali kuwa na azam tv iko powaa kuliko icho kifurushi chao
 

Ha ha ha Mkuu.. hizo zitaendelea kuwa chini ya kapeti.. Azam hawana ubavu huo wa kulipa abt Us $100,000,000 kwa ajili ya rights kuonyesha mechi za Premier League.. DSTV wana coverage kubwa sana tofauti na Azam..
 
Ukiona hivi wamekamatwa pabaya na ushindani wa kina Az, Star T, Cont na Dig...Jambo zuri likilocheleweshwa sana!

Good move for the pople of TZ. Will be there for inaguration promo. Good medicine for SINO (ST).


Watuambie kama zipo nternational news / za kimataifa ??BBC au CNN
 
swali kwako mkuu hua unaona channel ngapi za mpira i mean ligi ya Epl...na je kuna channel gan itaonesha big brother kwenye kifurushi hiko....nipe jibu nisije kufnya maamuzi yenye majuto Pumb

Mkuu MstahikiMeya.. Ili uone mechi zote unahitaji kuwa na DSTV Premium ambayo ni TShs. 142,000/= kwa mwezi.. Hapo utaona supersports zote pamoja na ss select.. Halafu kuna Compact plus ambayo ni Tshs. 92,000/=.. Hii unaona supersport 3 (ambayo ndo inaonyesha mechi zote kubwa).. supersports 7 ambayo inaonyesha mpira kama ikiwa mingi na supersports 9 ambayo ni kwa east africa na haswa ligi ya Kenya.. Hizo package nyingine zilizobakia hupati access ya kuona mipira ya ulaya na mashindano makubwa..

NB: Supersport hawaonyeshi mechi za qualifying Uefa Euro 2016.. Huo ni upungufu mkubwa sana na sijui walipigwa bao au..
 
Last edited by a moderator:
Hii ni habari njema ila nadhani basi azam ndio watapanda dau zaidi.
 
Ushindani unasiaidia sana maana hawa jamaa walikuwa wanatupiga mabei ya ajabu ajabu zamu yao kutengeneza faida kiasi cha Mboga.
PoleNI big bosses stiff competition is on the way zama za super profit zimeisha.
 

shukran mkuu sosoliso kwa jibu makini sasa nihivi SINUNUI bora AZAM
 
Last edited by a moderator:
Hii ni habari njema ila nadhani basi azam ndio watapanda dau zaidi.

Hata kama wakipanda bei, sidhani kama watatufanyia 142000 kwa mwezi. Sidhani! Ngoja tuone kama ni habari za kweli, ila ubavu Azam wa kununua rights wanao.
 

Mkuu, nimeangalia kwenye website yao wanasema kifurushi hicho cha Tshs 17,500 kitaonyesha channel za supersports select na supersports select 2. Channel hizi huwa zinaonyesha baadhi ya mechi za EPL, Champions League na baadhi ya mechi za ligi nyingine za Ulaya kama Serie A, Bundesliga na La Liga.
 
Azam tv hana ubavu wa kumnyang'anya tenda Dstv ya kuonyesha chanel za super sport. Walikuja wajerumani wa g-sport miaka ya 2000+ wakachukua tenda ya kuonyesha match za primier wakachemka. Hawakumaliza hata msimu mmoja wakawa wamefilisika.

Nawashangaa wabongo kwakulalamika eti dstv anatoza bei kubwa kwenye kifurushi cha primium. Sasa ulitarajia uangalie ligi za ulaya kwa kulipa buku 10??? Teteteteee.

We unadhani watu wanakurupuka wanaenda viwanjani kufunga kamera na kuanza kurusha match live bila mikataba na vyama vya mipira? Supersport analipa hela nyingi sana kununua haki za matangazo na maonyesho ya mipira naye anakuja anamuuzia Dstv ili amrushe live na dstv anakukamua wewe mlaji wa mwisho.... dstv imesambaa karibu afrika nzima tofauti na azam inayoishia mtukula unadhani akinunua mkataba wa dstv atakukamua sh ngap we mlaji, na ndo hivo hana wateja wengi. Mwisho wa siku ataambulia hasara takatifu kwani hata akiwatoza mara 2 ya zile za dstv yan tsh.300,000 kwa mwezi bado hawezi kuiepuka hasara kwasababu ana wateja kiduchu.

Otherwise mtakua mnajifariji na maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Aiseee mie ombi langu ni waache kututoza hiyo subscription fee kwa terms za dollar.. Inatuumiza sana.. Imagine DSTV Premium imeruka toka TShs. 135,000/= per month to TShs. 142,000/= just kwa sababu dola imepanda..!

Hii nchi ni hapo tu inapokera, utadhani tupo marekani kila kitu dola. Nawafute basi sarafu yetu ijulikane moja. Maana imekuwa kama vile nchi haina uongozi wa kukemea hili. Hawa Chadema bwana oooh sorry siyo chadema ni nanilii hawaa.......M wanakera sana wameshindwa kusimamia nchi
 
Hakuna jipya hapo. Package ya Access ipo siku nyingi kwa bei hiyo ilikuwa 16.5k nadhani baada ya dola kupanda ndo inakuwa 17.5k. Nadhani hii ni kwa wanataka kujiunga n not wateja wao wa zamani.
 
Hiyo 17,500/= ni pamoja na kodi (VAT), au kabla ya kuongeza kodi!
 
Hiyo 17,500/= ni pamoja na kodi (VAT), au kabla ya kuongeza kodi!
 

Kama ni hivyo hakijabadilika kitu, coz mpaka sasa package ya 17,500 ss select zinapatikana, ss9 na ssblitz...mechi nyingi za uefa za jumatano huwa wanaonyesha ss select, sema tu unaweza kukutana na mechi ambayo hukutaka kuangalia
 
Tatizo Shilingi yetu haina Thamani tena. Tusipopata viongozi wasomi wazalendo wenye mapenzi mema na hii nchi, basi tutegemee mporomoko huu wa Tsh zaidi na zaidi na mfumuko wa bei zaidi.

Ndugu yangu kwani mkuu wa kaya nae si ni msomi yule tena mchumi sasa unataka viongozi gani tena wasomi? naibu waziri wa fedha ni mchumi wa first class digrii ya udsm sasa sijui huyu nae sio msomi?
 

wacha wee...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…