“Walimu semeni shida zenu na wakati wote msijione duni, oneni namna Serikali inavyoweza kutatua changamoto zenu. Nataka niwakumbushe Watanzania kuwa ninyi ni nguzo ya taifa letu, zoezi hili linamfanya mwalimu mwenyewe kukutana na watoa huduma Serikalini ili kujua nini kitafanyika juu ya changamoto yake,” amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko ameyasema hayo mkoani Geita wakati aliposhiriki katika ‘Samia Teacher’s Mobile Clinic - Geita’ inayolenga kusikiliza na kutatua kero za walimu Mkoani Geita.