Dua maalum kwa taifa

Dua maalum kwa taifa

DENLSON

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
949
Reaction score
1,260
Ewe Mtanzania mwenzangu, nchi hii ni yetu tumepewa na Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi. Tumepewa iwe urithi wetu. Ni jukumu na wajibu wetu kuiombea mema na kuikinga na mabaya dhidi ya maadui wote wa nnje na ndani hivyo njoo tumuombe Mungu ailinde nchi yetu dhidi ya maadui na wabaya.

DUA

Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze, usinyamaze mbele ya maadui wa nchi yangu Tanzania, Uweke watu wakorofi juu yao, washitaki wasimame mkono wao wa kuume.

Siku zao na ziwe chache, Usimamizi wao na watwae watu wengine. Watoto wao na wawe yatima, Na wake zao na wawe wajane. Kutanga na watange watoto wao na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao.

Wadai na wanase vitu vyote walivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yao. Wasiwe na watu wa kuwafanyia fadhili, Wala watu wa kuwahurumia yatima wao. Wazao wao waangamizwe, majina yao yakafutwe katika kizazi cha pili.

Uovu wa baba zao ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya mama zao zisifutwe. Wakumbwe na aibu na fedheha, wanayoyapanga sirini yawe hadharani, vikao vyao viwe mafarakano na maamuzi yao yawe mabishano. Kwakuwa wewe Bwana umeipenda nchi yangu tangu kizazi na vizazi.

Maendeleo yaje kwa haraka, uwalinde viongozi wetu na kuwapa hekima wafanya maamuzi. Utunyeshee mvua zetu kwa wakati na jua kwa majira yake. Wana na binti zetu wale katika ardhi ya nchi yetu na wajukuu zetu wacheze katika ardhi uliyotupa kuimiliki.

Milima na itoe madini, mabondeni kipatikane chakula. Anga na izae ndege wa kila namna na Bahari samaki kwa aina zake. Mito itiririshe maji na misitu itupe asali Ee Bwana Uisimamishe Tanganyika, uifanye imara Zanzibar.

Amina
 
Back
Top Bottom