Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Dubai wamefanikiwa kuzindua kamera zenye Teknolojia ya hali ya Juu ya AI iliyoundwa ili kuweza kugundua ukiukaji wa sheria 17 za alama za barabarani, kuanzia watu ambao wako kwenye gari hawafungi mikanda ya usalama na injini za sauti zilizobadilishwa kinyume na sheria.
Kamera hizi za teknolojia ya juu hutumia picha ya infrared ili kunasa picha na video zilizo wazi, hata kupitia madirisha yenye rangi nyeusi, kuhakikisha utekelezwaji sahihi hata vioo vilivyo tinted.
Brigedia Mohammed Ali Karam wa Polisi toka Dubai alieleza kuwa mfumo huo unaweza kutofautisha kati ya nguo na mikanda ya usalama, hata katika mwanga mdogo. Pia hutambua matumizi ya simu ya mkononi wakati wa kuendesha gari kwa kuchanganua mienendo ya mikono, kusaidia kuzuia uendeshaji wa gari huku watu wanachati kupitia simu.
Teknolojia hiyo hutumia Rada kupima viwango vya kelele vya injini, ikitoa faini kwa magari yanayozidi desibel 95. Wahalifu wanaweza kukabiliwa na faini ya hadi Dh3,000, pointi nyeusi na kizuizi cha magari.
Mpango huu unaunga kuweza kuondoa ajali za kijingoa kwenye jiji la Dubai, kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuimarisha usalama barabarani. Wenye magari wanaweza kupinga faini kupitia programu ya Polisi ya Dubai, wakikuza uwazi na haki.