Dubai yasema iko tayari kutoa $6 Bilion (Tsh. 15T) kujenga Reli ya Kenya, Uganda na DRC kwa sharti la kuwa na mgao mkubwa Mombasa Port

Safi sana,na Wao Waarabu wanafaidika nini?
 
Safi sana,na Wao Waarabu wanafaidika nini?
Wao watapata pesa yaani wanaamini wakiwekeza watapata wateje wengi hivyo kinaweza kuwa na mgao wa 55(Mwarabu) Kwa 45(Tanzania)

Ni kama vile middleman atatafuta wateje Kwa niaba ya mwenye Mali
 
Tanzania ni shamba la bibi.Kule wanaomba share tu,na hela wanatoa. Kwetu tunawapa Bandari bureeeee,na hela za kuendeleza bandari TPA ndo wanatoa.Mkumbuke Serikali ilikopa ma trilion ya kuendeleza Bandari.
 
Wao watapata pesa yaani wanaamini wakiwekeza watapata wateje wengi hivyo kinaweza kuwa na mgao wa 55(Mwarabu) Kwa 45(Tanzania)

Ni kama vile middleman atatafuta wateje Kwa niaba ya mwenye Mali
Ok kwa yale uliyosema hapo juu kama faida kwa Wa Tanganyika,Je kuna ulazima wa Waarabu au unadhani kuna mahali sisi kama Taifa tunakosea?Kama tukijipanga tutafaidika wenyewe kwa hiyo 55% +45% kubakia ndani?
Binafsi kwa sababu ulizozitoa wewe naona bado tunauwezo kama tukijua tatizo lilipo nakuweka mambo yetu sawa.
 
Jirani akijiuza au akitoa uroda na Sisi tufanye vivyo hivyo
 
Kwamba kenya ikiamua inashindwa ku-raise hizo pesa ?!!!!

Hii generation ina viongozi wapuuzi sana (The Pan-Africanist of yesteryear wangekuwepo bado hai wangekufa kwa mshituko)
 
Ulazima usingekuwepo hizo kero zingekuwa zimeshakwisha ila Mali ya Umma ni shamba la bibi
 
Ulazima usingekuwepo hizo kero zingekuwa zimeshakwisha ila Mali ya Umma ni shamba la bibi
Sasa ndio tuanzie kwa tatizo lilipo,
Bora hata tuajiri hao waarabu munaodhani watafanya vizuri kwenye Utawala na Wataalamu.
Kama tunaamini wapo vizuri nibora hata watupatie wataalamu wao kwamuda,watunyooshee palipo na udhaifu then baada ya miaka kadhaa watuachie Bandari na Wataalamu Wazalendo watakao watengeneza.
 
Shida ni fikra za kimaskini, mtu hana na hajui hana kwanini!
 
Sio swala la kudhani watafanya vizuri tayari wanafanya hivyo kwenye Nchi kibao tuu
 
Wacha wachamkie ila Tz siye Bado na hatutaki
 
Tanzania ni shamba la bibi.Kule wanaomba share tu,na hela wanatoa. Kwetu tunawapa Bandari bureeeee,na hela za kuendeleza bandari TPA ndo wanatoa.Mkumbuke Serikali ilikopa ma trilion ya kuendeleza Bandari.
Kaka! Kule wanaomba share au wanajenga reli kwanza?! Gharama zilizotajwa ni za ujenzi wa reli, na Tanzania hatuna deal ya aina hiyo. Tanzania inataka kuboresha utendaji kazi wa bandari sasa hapo share au sio share itatajwa mbele!
 
Pesa hizo ni ndogo sana. Yaani unachachawa na 15t tu.

GDP ya Tanzania ni zaidi ya Tsh 180t.

Usituletee ukoloni mambo leo hapa.
 
Kama wanataka kujenga huko kenya wajenge tu. Hatuwezi kufanya maamuzi kwa kuiga majirani.

Soko letu la ndani na nchi kadhaa za SADC linatosha kabisa.
 
Pesa hizo ni ndogo sana. Yaani unachachawa na 15t tu.

GDP ya Tanzania ni zaidi ya Tsh 180t.

Usituletee ukoloni mambo leo hapa.
Sasa hapa ndio umeandika nini? Hoja ni kwamba Dubai wakishika Mombasa Port na nyie mkabakia na urasimu wenu Dar Port itaishia kuwa tembo mweupe so hoja sio reli Bali Mombasa Port
 
Kama wanataka kujenga huko kenya wajenge tu. Hatuwezi kufanya maamuzi kwa kuiga majirani.

Soko letu la ndani na nchi kadhaa za SADC linatosha kabisa.
Mawazo ya watu walioshiba vya Bure na Kodi za maskini huko Ikulu.

Wapuuzi kama nyie ndio mlikuwa mnashangilia wakati Tanzania na Kenya wanafungiana mipaka wakati mazao ya wakulima yanaoza na hakuna mnachofanya Kwa sababu nyie mnapata vya Bure huko Serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…