Dubai yasema iko tayari kutoa $6 Bilion (Tsh. 15T) kujenga Reli ya Kenya, Uganda na DRC kwa sharti la kuwa na mgao mkubwa Mombasa Port

Serikali za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na DRC kwa pamoja zimeshindwa kujenga reli ya kisasa kurahisisha usafirishaji kati yao wenyewe mpaka ziende kusubiri masharti magumu?
 
siyo kweli mkuu. DRC kwa mfano, ni nchi kubwa sana; Kenya haiwezi kuihudumia drc yote, hata Tanzania haiwezi kuihudumia yote. Kenya anaweza akaihudumia kuanzia kaskazini mpaka pengine kivu ya kusini tu inayopakana na rwanda. Hata hiyo Kivu ya kusini si ajabu wakapendelea kuhudumiwa na bandari ya Dar kutokana na umbali kutokea mombasa.

Kuanzia kivu ya kusini mpaka kusini kabisa katanga/lubumbashi mpaka mpakani na zambia hiyo ni teritory ya tz, piga ua.
Hata rwanda pia ni mbali kutokea mombasa ukilinganisha na dar. cha msingi serikali ihakikishe sgr inakamilika, kwa sababu rwanda na uganda wanapenda wawe na option zote mbili.- mombasa na dar.
 
Hizi mada zote ni kutetea DPW, kwani hatuna akili zetu mpaka tufanane na Kenya πŸ‡°πŸ‡ͺ
Dipiwold waje ila MKATABA...
 
Sasa hapa ndio umeandika nini? Hoja ni kwamba Dubai wakishika Mombasa Port na nyie mkabakia na urasimu wenu Dar Port itaishia kuwa tembo mweupe so hoja sio reli Bali Mombasa Port
Sasa shida ni nini wakishika Bandari ya Mombassa?

Washike tu. Yaani unatutisha na kanchi kenye population ya watu 3m. Yaani United Emirates population yake ni 3m.

Mzee wao wafanye yao na sisi tutafanya yetu.

15tr ni ndogo mno. Ni kichaa pekee anaweza sign mikataba ya kijinga hivyo.
 
Wana pesa wewe mwenye lundo la maskini unafaidika na kipi? πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Serikali za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na DRC kwa pamoja zimeshindwa kujenga reli ya kisasa kurahisisha usafirishaji kati yao wenyewe mpaka ziende kusubiri masharti magumu?
Mpaka zirubuniwe!!!!!.......
 
Sasa shida wapi mdogo wangu. Sasa kama kenya wanafanya upumbavu tuwaache tu eti kwa sababu ni majirani? Stupid ideas.

Yaani mawazo yako ya kitoto kabisa. Unachachawa na 15tr. Mzee hii nchi ya Tanzania ipo tu. Tumeikuta na tutaiacha. Hatuwezi kufanya maamuzi kwa njaa zenu hizo.

Kama bandari haitafanya kazi miaka hii, Itafanya kazi in future.
Bahari haihami mdogo wangu
 
Hakuna upumbavu wanafanya wanaenda kupokonya share kubwa ya Bandari ya Dar ,mkivimbiwa mjue Kuna wengine Wana njaa wanahitaji pesa
 
Great work. πŸ‘
 
Kama hujaiona kupitia michango ya wadau humu, piga filimbi.
Ndio mkipewa nafasi mnauza kila kitu.
Sisi tunashauri uwekezaji mkibwa uje,ila tushirikishwe wananchi.
Tanzania yetu 🎡 🎢
Huna akili bwana usitubabaishe hapa ,ujima and local minded
 
Wana pesa wewe mwenye lundo la maskini unafaidika na kipi? πŸ˜‚πŸ˜‚
Umaskini ni wetu. Lakini tupo na resources kuwazidi hao ndugu zako toka mashariki ya kati.

Resources zipo tutazilinda for our future generation.

Unadhani baada ya mafuta kuisha au kupungua kwa matumizi duniani hao ndugu zako kutoka Dubai watapata wapi source of income?
 
Nimekwambia tumia akili.

Kenya hawajaingia hata hiyo IGA lakini wametanguliziwa offer ya tri 15,

Huku Hadi IGA inasainiwa mwaka sasa lakini hakuna popote imeandikwa watatoa hata 100 mbovu!!
Basi Kenya ni wajanja sana.

Watowe "100 mbovu" ya nini?
 
Kwani Kenya wameshakubali mkuu?

Huyu ChoiceVariable ni wale kundi la chawa wa mama

Habari kama hizi anazipenda ili kuwafanya Watanzania tukubali mkataba wa DPW

Hizi ni mbinu zao za kisaikolojia
 
Kama hujaiona kupitia michango ya wadau humu, piga filimbi.
Ndio mkipewa nafasi mnauza kila kitu.
Sisi tunashauri uwekezaji mkibwa uje,ila tushirikishwe wananchi.
Tanzania yetu 🎡 🎢
Nyie si ndiyo wa kwanza mnawapokea wageni kwa ngoma pale eyapoti?

Ushirikishwe vipi zaidi?
 
Mdogo wangu hao Dubai wapo wanajua siyo mda mrefu uchumi wao unakufa. Kwahiyo wanatafuta makoloni ili kuweza survive.

Ungesoma kuhusu kupanda na kuporomoka kwa uchumi wa Nauru, ungelipata somo vizuri.

Hawa Dubai ni mifano ya Nauru.
Uchumi wa Dubai unategemea nini?

hata siafu wanatafuta makoloni mapya kila kukicha, cha ajabu nini Dubai Dubai wakitafuta makoloni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…