Dude akiri kubebeshwa madawa ya kulevya

Dude akiri kubebeshwa madawa ya kulevya

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801

dude.jpg

Stori: Gladness Mallya

STAA wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude' amekiri kubebeshwa madawa ya kulevya bila kujua na kujikuta akiponea chupuchupu kutokana na umaarufu wake.

DUDE200.jpg

Kulwa Kikumba ‘Dude'.

Akizungumza na paparazi wetu, Dude alisema amewahi kubebeshwa unga na rafiki yake wa karibu ambaye hakumtaja jina na walikuwa wakitokea Nairobi nchini Kenya kuja Tanzania.Alisema wakati wanaanza safari alipewa koti la baridi na rafiki yake huyo, akalivaa kumbe ndani yake lilikuwa limeshonewa pakti za unga.

Walisafiri kwa gari na kila walipokutana na polisi wanaokagua hawakumkagua Dude kwani waliishia kupiga naye picha na kumsifia kwa kazi yake mpaka alipofika jijini Dar es Salaam.

"Kila tulipokuwa tunakutana na polisi rafiki yangu alikuwa akiwawahi na kuwaambia kwamba yupo na mimi ambapo walifurahia kuniona na kupiga picha na mimi bila kunikagua chochote," alisema
Dude.

Baada ya kupita vizingiti vyote, waliingia jijini Dar es Salaam maeneo ya Kinondoni Manyanya alipokuwa akiishi rafiki yake huyo ambapo alimwambia avue koti, akaanza kufungua mzigo aliokuwa ameushonea kwa ndani.

Dude alijikuta akishikwa na tumbo la kuhara kutokana na mshtuko alioupata baada ya kuona rafiki yake huyo akitoa madawa ya kulevya.

"Jamaa alinipa shilingi elfu hamsini za Kenya na ni baada ya kufika Dar ndipo niligundua kwamba nilikuwa nimebebeshwa unga lakini yule jamaa alishakamatwa na anatumikia kifungo nchini Pakistani," alisema Dude.

Hata hivyo Dude aliwashauri mastaa wenzake kuwa makini na marafiki zao kwani siyo wote wanaokamatwa wamebeba unga kwa kujua bali wengine wanabebeshwa tu bila kujua.

Kama kapokea hizo 50,000 basi ni muongo, walishirikiana.

Kama kweli alikuwa hataki kubebeshwa unga na kabambikiwa kwani asimshtaki huyo rafiki yake hapo hapo na kizibiti kipo? kuna urafiki katika kupotezeana maisha?
 
Mwongo. Kama alikubebesha bila kujua alikuwa na sababu gani kufungua mbele yako ili ujue? Ili ukamshtaki ? Ili akulipe hela? Uongo mwingine wa kitoto sana....
 
Uongo ukizidi sana unakuwa ukweli..Sasa ndiyo atabebeshwa..
 
Hivi habari za magazeti ya udaku nazo zinakuja jukwaa hili?
 
Kwenye nchi za watu, huyu kwa sasa angeguswa na mkono wa sheria katika macho ya criminality. He's accessory under Criminal Law. He has contributed to or aided in the commission of a crime hasa baada ya kukubali kupokea Ksh 50,000 na kukaa kimya.

Huwezi kugundua kama ulikuwa umebeba madawa ya kulevya halafu ukapewa Ksh 50,000 na kuamua kukaa kimya mpaka aliyekupa akakamatwa na madawa mengine ndiyo ukaamua kutoa habari kwenye jamii.

Kwanza kupokea tu hizo pesa ni kosa la jinai achilia mbali kutokutoa taarifa polisi ya kile kimetokea kwa kukuhusisha bila 'kufahamu'.

Kwa Tanzania inaweza isionekane kama ni kosa la jinai lakini hata kiroho, huwezi kukubali kulipwa kwa kubeba silaha ambayo unafahamu inaenda kuua watu halafu ukasema poa tu. This is ludicrous to say the least.

Kweli Tanzania siyo kama tuijuavyo wapita njia.
 
Dude mwongo kama kweli akujuwa kwa nn asimtaje kws ss ilhali jamaa yupo jela?usaniii
 
Huyo ndiye Yahaya...kamba kwake kawaida akawafunge kamba mapimbi wenzie huko.
 
Alichoongea Dude ni uongo wa dhahiri.

Kama jeshi letu la polisi lingekuwa linafanya kazi yake kwa weledi, ilibidi mara tu gazeti hilo lillipoanza kusambazwa kwa wasomaji, huyo jamaa awe keshakamatwa na polisi, kufanya formality ya kukamilisha upelelezi wao, ili ifuate hatua ya kumburuza mahakamani.

Upo ushahidi usio na mashaka yoyote kuwa Dude alishirikiana na huyo mtu ambaye hakutaka kumtaja jina, kuuvusha huo 'unga' toka Kenya kuja TZ, hasa hasa ushahidi wenye nguvu hapo ni yeye mwenyewe anakiri kuwa alipewa pesa elfu 50 ya Kenya na akakaa kimya.

Nitawashangaa sana polisi wetu, hasa kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya, kama wataamua kulikalia kimya suala hili, bila kumkamata Dude, wala kuitolea ufafanuzi stori hii, ambayo ameitoa mwenyewe Dude kwa hiari yake, bila kulazimishwa na mtu yeyote!!
 
Duh....hili DUDE ongo kama nini..............

Kesho atakuja kutuambia kuwa aliwahi kumkuta rafiki yake chumbani na mkewe, akapewa laki tano akapoa.......

Mtondogoo.....atatuambia, siku moja nilikuwa na jamaa yangu tumelala...nikashtuka usiku wa manane nikamkuta ananipapasa maka.a.l.i.o.....akanipa buku tano nikarudi zangu kulala.
 
Kwenye nchi za watu, huyu kwa sasa angeguswa na mkono wa sheria katika macho ya criminality. He's accessory under Criminal Law. He has contributed to or aided in the commission of a crime hasa baada ya kukubali kupokea Ksh 50,000 na kukaa kimya.

Huwezi kugundua kama ulikuwa umebeba madawa ya kulevya halafu ukapewa Ksh 50,000 na kuamua kukaa kimya mpaka aliyekupa akakamatwa na madawa mengine ndiyo ukaamua kutoa habari kwenye jamii.

Kwanza kupokea tu hizo pesa ni kosa la jinai achilia mbali kutokutoa taarifa polisi ya kile kimetokea kwa kukuhusisha bila 'kufahamu'.

Kwa Tanzania inaweza isionekane kama ni kosa la jinai lakini hata kiroho, huwezi kukubali kulipwa kwa kubeba silaha ambayo unafahamu inaenda kuua watu halafu ukasema poa tu. This is ludicrous to say the least.

Kweli Tanzania siyo kama tuijuavyo wapita njia.
Kweli yaani hii nchi sijui kwakweli huyu tayari anaweza kupapaswa vizuri maana alibeba.
 
Zunga tu!

Tulikuwa tumekusahau leo nimekukumbuka hivi wewe una igiza eeh?
 
Hamna polisi wasomi wanaopita humu jf..nadhani dude ana zaidi ya alichoongea. Tuanzie hapo
 
Kama kapokea hizo 50,000 basi ni muongo, walishirikiana.

Kama kweli alikuwa hataki kubebeshwa unga na kabambikiwa kwani asimshtaki huyo rafiki yake hapo hapo na kizibiti kipo? kuna urafiki katika kupotezeana maisha?

Hela ni kitu kingine mkuu
 
Back
Top Bottom