Dudu Baya azunguza juu ya mwanae kuacha shule na kuanza kuimba muziki

Dudu Baya azunguza juu ya mwanae kuacha shule na kuanza kuimba muziki

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari wadau wa celebrity Forum.

Niende madani hapo juu. Mmoja wa wasanii wakongwe ktk fani hususan Bongo fleva, Dudu Baya aka Dudu Zuri amehojiwa na sudi Brown wa clouds FM juu ya kumtelekeza mwanae wa kiume aitwaye William mwenye miaka 17.

Ktk mahojiano hayo kupitia shilawadu, Dudu alidai hajamtelekeza William ila alikuwa akituma matumizi na kila kitu cha shule ila alishangaa kusikia mtoto ameacha shule na kuanza kujishughulisha na muziki.

Alimlaumu mamake mtoto kuwa akituma hela kwa mtoto zilikuwa hazimfikii mtoto na badala yake alikuwa akila matumizi ya mtoto pamoja na bibi yake. Alisema kutokana na hali hiyo mtoto aliamua kuacha shule kwani Dudu alikuwa akipigwa vizinga kupitia William.

Alimshangaa pia William kuimba muziki lakini hakuwahi kutafuta ushauri kwake ilihali anajua yeye ni nguli wa muziki wa kizazi kipya. Alimpongeza kwa kuacha shule badala angetumia hela nyingi kumsomesha kumbe kichwani hakuna kitu.

Sudi mwishoni alimsikilizisha Dudu wimbo wa William na Dudu aliufurahia sana na kusema ni bonge la ngoma. Anaendelea kumuasa William aende kutafuta ushauri kwake kwani kawaunganisha chipukizi kibao na wadau mbalimbali wa Muziki. Jina lake la kisanii ni William Dudu.
 
Dudu Bata katisha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
😀😀😀 kuna baadhi ya wasanii unaweza sema zamani waliingiwa na pepo wa kuimba, sahivi pepo katoka, maana hata hawajielewi
 
Huyu Baba ndo alipaswa kurudi Shule.., mana inaonekana hajitambui kabisaa!!!
 
Katika watu waliokosea mahusiano..ni sugu kwa faiza....na mama william kwa dudu baya.....wanajuuta kuwazalishana na wenza wao
 
watu mnamshangaa dudu baya wakati huyo mtoto ndo alikataa shule akakimbia home..mbona hiyo story tu yan mmeikutia mwisho halaf mnaanza kumjudge vibaya dudu baya..Watanzania hii tabia mtaacha lini
 
Huyo mtoto namkumbuka sana hasa kwenye wimbo wa dudubaya -nimeaondoka,
 
Back
Top Bottom