Dudu Baya: Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benzi, acha afe

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Msanii mkongwe wa muziki, Dudu Baya, amesema hawezi muomba msamaha Chidi Benz kutokana na kauli yake ‘acha afe’ ambayo aliitoa baada ya rapa huyo kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya na kuomba msaada.

Msanii mkongwe wa muziki, Dudu Baya, amesema hawezi muomba msamaha Chidi Benz kutokana na kauli yake ‘acha afe’ ambayo aliitoa baada ya rapa huyo kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya na kuomba msaada.

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya amesema aliitoa kauli hiyo baada ya kuona rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa na watu ambao walijitokeza kumsaidia.

“Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benz kwa kauli yangu ya acha afe,” alisema Dudu Baya “Nachoweza kufanya ni kumpa pole kwa matatizo yaliyompata, na ninamwombea dua Mungu ampe nguvu mpya, akili mpya, mwanga mpya. Bongofleva inamwitaji, jamii imemmis, familia yake inamwitaji na inamtegemea. My best rapper, my friend Chidi Benz hakuna wa kukuokoa, jiokoe,”

Chizi Benz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukubali kupelekwa Bagamoyo Sober House kumsaidiwa kuondokana na matatizo yanayomkabili.

Source: Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benz kwa kauli yangu ‘acha afe’ – Dudu Baya | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Dudu linatapatapa halina hata single moja, Kazi kufatilia maisha ya wenzake
 
Yeye mwenyewe kashavurugwa anaitaji kwenda sober house. Tayari kashavurugwa tayari
 
Anahisi kifo ni adhabu anasahau kua kifo ni wajibu kwa kila MTU, kila MTU lazima afe kwa njia atazoamua mwenye mamlaka
 
Chomeka mzizi... haloo baby.....dudu baya bana alikuwa mjinga sana....he was doing better si ashushe ngoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…