Dudubaya ampa kichapo mkubwa mmoja wa polisi jijini Mwanza

Dudubaya ampa kichapo mkubwa mmoja wa polisi jijini Mwanza

Skype

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
7,266
Reaction score
1,633
Wadau poleni na majukumu ya hapa na pale katika kupambana na maisha ili kuweza kujipatia kipato. Wakati taifa likiwa limeingia uhasama kati ya wanchi na majeshi ya ulinzi, zimenifikia taarifa kutoka Mwanza kua mwanamuziki wa nyimbo za kiswahili Tanzania bwana Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya amempa kichapo mkubwa mmoja wa polisi jijini humo.

Habari zaidi zinatonya kua wiki iliyopita mwanamuziki huyo alikua na rafiki zake kwenye ukumbi mmoja wa starehe mida ya usiku wakijiburudisha na kubadilishana mawazo ya hapa napale, ndipo akaibuka mkubwa mmoja wa polisi na kusalimiana na hao rafiki zake (rafiki za Dudubaya). Katika mazungumzo wakamtambulisha mkubwa huyo kua wapo pia na rafiki yao (Dudubaya) ambaye ni mwanamuziki. Ghafla mkubwa huyo alianza kutoa maneno ya kashfa kwa mwanamuziki huyo akidai kua wala hafahamiani na watu mafala kama hao.

Kitendo hicho kilimkera sana Dudubaya na kuamua kumkunja vilivyo mkubwa huyo. Baada ya siku kama 2 au 3 Dudubaya akasafiri kuelekea Shinyanga kibiashara na baadae kwenda Dar ambapo mpaka naripoti mda huu yupo huko.

Kutokana na kichapo hicho mkubwa huyo amekua akizunguka na defender akimsaka Dudubaya pasipo kujua kua kwa sasa hayupo jijini Mwanza. Leo Dudubaya akihojiwa na vituo vya redio jijini Dar es salaam amesema, "Huyo mkubwa amezowea kunyanyasa raia, nilimkunja kwa sababu hana adabu na ndiyo maana wanachukiwa na raia, hata mimi nikisikia kuna majambazi siwezi kushirikiana na polisi kuwapa taarifa maana wao ndo wamekua watesaji wa raia na nampa taarifa kama nikikutana nae akiwa na mambo hayohayo ya kijinga kinanuka tena na namwambia hawezi kunifanya kitu"

Ni hayo tu ndugu zanguni.

source: kituo cha redio cha Times FM.

My take:

Kwa taarifa hii inaonekana sasa uhasama umetamalaki kati ya wananchi na majeshi ya ulinzi na usalama, inabidi watawala wafanye juhudi kurejesha imani kwa raia vinginevyo kila mtu atajichukulia sheria mkononi hatimaye tutaishi kwa kuwindana kati ya familia za kiraia na zile za kijeshi (polisi, magereza, jwtz).
 
uyo polis alikunjwa kwenye ulevi na starehe. hivo achukulie poa tu akuwa kazin na pengine alikuwa yuko tungi kwa pombe hivo awe mdogo tu
 
hahaha kumbe the dudu bado anagawa vichapo tu,safi sana umenifurahisha kwa kumkunja huyo ----
 
hahaha kumbe the dudu bado anagawa vichapo tu,safi sana umenifurahisha kwa kumkunja huyo ----

Godfrey Tumaini ndo jina lake ila aka zake sasa aaaaa...

Dudubaya

Mamba

Manundu

Ngumi mkononi

......
 
hili la kukataa kushirikiana na Polisi kuhusu ujambazi siyo uamuzi mzuri. ......
 
hili la kukataa kushirikiana na Polisi kuhusu ujambazi siyo uamuzi mzuri. ......

Mkuu TANMO, hivi siku hizi kuna tofauti yoyote kati ya jambazi na askari?

Kuna mama kule Mtwara alikamatwa na askari (polisi) akabakwa, akapigwa risasi akauawa, je kitendo hiki kina tofauti yoyote na kitendo cha jambazi? Hapo tu kwanza mkuu.
 
Last edited by a moderator:
soggy dogy alishasema kua wizari ya ulinzi nimteua dudu baya mapromota matapeli watapewa kichapo cha mbwa koko by the way polinyinyiem piga tu hawana adabu.
 
Hahahaha nicheke mie niongeze siku. Siku hizi mnapigana na raia? Basi kwisha kazi yenu nyie polisi.
 
Hahahaha nicheke mie niongeze siku. Siku hizi mnapigana na raia? Basi kwisha kazi yenu nyie polisi.

Polisi ni majambazi na majambazi ni polisi, kwa hiyo hatuna walinzi wa raia na mali zao bali vibaka, wanyang'anyi, watesaji, wauaji, etc etc.
 
Mkuu TANMO, hivi siku hizi kuna tofauti yoyote kati ya jambazi na askari?

Kuna mama kule Mtwara alikamatwa na askari (polisi) akabakwa, akapigwa risasi akauawa, je kitendo hiki kina tofauti yoyote na kitendo cha jambazi? Hapo tu kwanza mkuu.

Mkuu wangu Skype nakubaliana na wewe kuwa hawa Jamaa wakati mwingine wanashindwa kujitofautisha na Wahalifu,,,,,
Lakini unapofanikiwa kugundua wahalifu wanaotaka kufanya tukio la uhalifu mahali utaacha kuwashtua Polisi eti kwa sababu unawachukia Polisi? Vipi kuhusu watakaoathirika na huo uhalifu?
 
sasa si anamaliza mafuta tu na hiyo defender
kumsaka dudubaya!!!!

si alisema hamjui nadhani kwa sasa atakuwa anamfaham vizuri sana
na hatohitaji utambulisho
 
Mkuu wangu Skype nakubaliana na wewe kuwa hawa Jamaa wakati mwingine wanashindwa kujitofautisha na Wahalifu,,,,,
Lakini unapofanikiwa kugundua wahalifu wanaotaka kufanya tukio la uhalifu mahali utaacha kuwashtua Polisi eti kwa sababu unawachukia Polisi? Vipi kuhusu watakaoathirika na huo uhalifu?

Mkuu najua una lengo zuri tu la kutaka kuiona jamii ikiwa na ushirikiano na majeshi yetu ila kwa sasa tulipofikia si pazuri kiusalama.

Sawa unaripoti tukio la majambazi polisi, watuhumiwa wa ujambazi wanakamatwa lakini baada ya siku chache unawaona wakitamba mtaani, sidhani kama utajisikia vyema.

Kuna wakati raia tunakosa amani kwa kuonewa na mapolisi mfano ukiangalia sakata la walalahoi Mwanza, Mbeya na Dar utaona ni uonevu. Leo unanifukuza nisifanye biashara zangu ndogondogo lakini kesho unalipwa mshahara kutokana na kodi yangu, vipi nitakufurahia? Sitaki kutaja habari za Ulimboka, Kibanda, Mwangosi na wengineo ila inaumiza kimwili na kiakili.

BTW watawala wayatumie majeshi yetu kulinda amani badala ya kuvuruga amani, hapo tutaelewana ila kwa sasa hali tuliyofikia si njema.
 
Kwa mujibu wa maelekezo ya Pinda,Dudu baya kaamua kupiga kabla hajapigwa!
 
Back
Top Bottom