Wadau poleni na majukumu ya hapa na pale katika kupambana na maisha ili kuweza kujipatia kipato. Wakati taifa likiwa limeingia uhasama kati ya wanchi na majeshi ya ulinzi, zimenifikia taarifa kutoka Mwanza kua mwanamuziki wa nyimbo za kiswahili Tanzania bwana Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya amempa kichapo mkubwa mmoja wa polisi jijini humo.
Habari zaidi zinatonya kua wiki iliyopita mwanamuziki huyo alikua na rafiki zake kwenye ukumbi mmoja wa starehe mida ya usiku wakijiburudisha na kubadilishana mawazo ya hapa napale, ndipo akaibuka mkubwa mmoja wa polisi na kusalimiana na hao rafiki zake (rafiki za Dudubaya). Katika mazungumzo wakamtambulisha mkubwa huyo kua wapo pia na rafiki yao (Dudubaya) ambaye ni mwanamuziki. Ghafla mkubwa huyo alianza kutoa maneno ya kashfa kwa mwanamuziki huyo akidai kua wala hafahamiani na watu mafala kama hao.
Kitendo hicho kilimkera sana Dudubaya na kuamua kumkunja vilivyo mkubwa huyo. Baada ya siku kama 2 au 3 Dudubaya akasafiri kuelekea Shinyanga kibiashara na baadae kwenda Dar ambapo mpaka naripoti mda huu yupo huko.
Kutokana na kichapo hicho mkubwa huyo amekua akizunguka na defender akimsaka Dudubaya pasipo kujua kua kwa sasa hayupo jijini Mwanza. Leo Dudubaya akihojiwa na vituo vya redio jijini Dar es salaam amesema, "Huyo mkubwa amezowea kunyanyasa raia, nilimkunja kwa sababu hana adabu na ndiyo maana wanachukiwa na raia, hata mimi nikisikia kuna majambazi siwezi kushirikiana na polisi kuwapa taarifa maana wao ndo wamekua watesaji wa raia na nampa taarifa kama nikikutana nae akiwa na mambo hayohayo ya kijinga kinanuka tena na namwambia hawezi kunifanya kitu"
Ni hayo tu ndugu zanguni.
source: kituo cha redio cha Times FM.
My take:
Kwa taarifa hii inaonekana sasa uhasama umetamalaki kati ya wananchi na majeshi ya ulinzi na usalama, inabidi watawala wafanye juhudi kurejesha imani kwa raia vinginevyo kila mtu atajichukulia sheria mkononi hatimaye tutaishi kwa kuwindana kati ya familia za kiraia na zile za kijeshi (polisi, magereza, jwtz).