Duh! bora hili la kuwaita Warundi waje kuilima Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hatua hii ni bora maana ardhi yote hiyo imewashinda kuilima, full majungu, mdebwedo na dezo dezo tu....

---------------------------------------------------------

Idara ya Uhamiaji nchini imeweka utaratibu wa kutoa kibali maalum kwa raia wa Burundi ambao wanataka kuja nchini kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo ikiwa ni moja ya nia za kupunguza raia wa nchi hiyo ambao huingia nchini kinyemela hususani katika mikoa ya Kigoma na Tabora kwa ajili ya kufanya kazi za kilimo kama vibarua.

Mpango huo umetangazwa na Kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini Dk.Anna Makakala mwishoni mwa ziara yake iliyomfikisha katika wilaya zote na katika maeneo ya mpaka na nchi jirani  mkoani Kigoma ambapo amesema vibali hivyo vya miezi mitatu vitawezesha raia hao kutambuliwa na serikali kupata fedha na kutambua wako wapi na idadi yao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema uamuzi huo wa idara ya uhamiaji utasadia kupunguza uhalifu na kuongeza tija katika kilimo pamoja na kujenga mahusiano mazuri na nchi jirani ya burundi ambayo raia wake wanaongoza kwa kuja nchini kufanya vibarua bila ya kibali na hivyo kuongeza idadi ya wahamiaji haramu.

Uhamiaji kutoa vibali maalum kwa Warundi.
 
Dah alafu kuna watu wanasema wana maisha magumu,.Alafu ndiyo naikumbuka ile methali isemayo"ukiona kwako kwaungua basi kwa mwenzio kunateketea"hakuna jinsi wacha tuwasaidie ndugu zetu waburundi.
 
Tusifurahie, kwa jinsi tulivyo mazuzu, Hawa Leo wanakuja kama vibarua Na baada ya muda mfupi wao ndio watakuwa wamiliki wa ardhi

Sasa kaka mumeshindwa kulima, mapori yote hayo, subiri mijitu ya Kirundi ije kuyapiga majembe muone Tanzania ikizalisha chakula kinachoweza kuuzwa Afrika yote.
 
waje nawakenya tuwape vibarua vya kulima mashamba tz@,nahitaj wakenya 15 waje mbeya region kunilimia shamba language@ I will pay them 100U S$ per actre
 
Sasa kaka mumeshindwa kulima, mapori yote hayo, subiri mijitu ya Kirundi ije kuyapiga majembe muone Tanzania ikizalisha chakula kinachoweza kuuzwa Afrika yote.

Wee unafahamu scale ya kilimo itakayofanywa na warundi?
 
Hawaji kuwekeza,ni cheap labors sana pale kigoma. Serikali ikizuia, mashamba mengi hufungwa
 
Sasa kaka mumeshindwa kulima, mapori yote hayo, subiri mijitu ya Kirundi ije kuyapiga majembe muone Tanzania ikizalisha chakula kinachoweza kuuzwa Afrika yote.
Wanakuja kufanya "vibarua" maana yake wanalima mashamba ya wenyeji na kulipwa ujira (kwa mujibu wa bandiko lako na nilivyoelewa)
 
Sasa kaka mumeshindwa kulima, mapori yote hayo, subiri mijitu ya Kirundi ije kuyapiga majembe muone Tanzania ikizalisha chakula kinachoweza kuuzwa Afrika yote.
Hujui hata kiswahili, unajua maana ya neno kibarua.?
 
Hujui hata kiswahili, unajua maana ya neno kibarua.?

Haijalishi, mwisho wa siku wao watalima hata kwa kujificha kwa kutumia mgongo wa neno vibarua, hiyo ni lugha ya kuficha aibu.
 
Haijalishi, mwisho wa siku wao watalima hata kwa kujificha kwa kutumia mgongo wa neno vibarua, hiyo ni lugha ya kuficha aibu.
Hamna mgeni anaeweza kupewa ardhi huku hii sio kunya hao wanakuja tu kua vibarua wetu walime mahindi ya kuwauzia huko maana wengi walikua wanaingia kwa njia za panya na kuja kusaka vibarua huku
 
waje nawakenya tuwape vibarua vya kulima mashamba tz@,nahitaj wakenya 15 waje mbeya region kunilimia shamba language@ I will pay them 100U S$ per actre
Ndio maana mliwafukuza wakenya na matrekta yao pale mpakani na Narok County? Mnawaza kulima kwa majembe kwenye karne hii utadhani ndio mnaiga yale ya Vasco Da Gama, R.I.P. Yaani ni ajab! 😀
 
Mijamaa ina nchi yao ila inaishi kama wakimbizi
 
Ndio maana mliwafukuza wakenya na matrekta yao pale mpakani na Narok County? Mnawaza kulima kwa majembe kwenye karne hii utadhani ndio mnaiga yale ya Vasco Da Gama, R.I.P. Yaani ni ajab! 😀
Huku kila mtu anajinafasi uamuzi ni wako tu mwisho wa siku unakula pesa za kuuzia nyang'au mahindi
 
Huku kila mtu anajinafasi uamuzi ni wako tu mwisho wa siku unakula pesa za kuuzia nyang'au mahindi
Mahindi ya Tz hayauzwi tena Kenya. Jiwe alitoa agizo. Hata hilo hujui, wewe ni mrundi pia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…