Mvutakamba
Member
- Jul 31, 2009
- 58
- 1
Katibu UVCCM apata wakati mgumu kesi ya Sendeka
Na Mussa Juma, Arusha
KATIBU wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Wilaya ya Monduli, Mathias Mihayo (43) ambaye ni Shahidi wa nne katika kesi shambulio na kutishia kwa silaha inayomkabili Mbunge wa Simanjiro Christopha Ole Sendeka(CCM) jana alipata wakati mgumu mahakamani baada ya kudai alijiunga na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) akiwa na miaka 12.
Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, James Kalehemaha katika kesi hiyo inayohudhuriwa na mamia ya watu, Shahidi huyo alisema ana umri wa miaka 43 na alijiunga na JKT mwaka 1978.
Akihojiwa na mawakili wa utetezi, Mihayo alisema alizaliwa mwaka 1966 na alimaliza darasa la saba mwaka 1976 katika shule ya Msingi Solwa Mkoani Shinyanga na mwaka 1978 alijiunga na JKT kambi ya Makotopola mkoani Dodoma.
Sehemu ya mahojiano baina ya Mawakili wa Utetezi, James Ngaro, Hezra Mwaluko na Mpaya Kamara na Shahidi huyo yalikuwa ni hivi.
Wakili Ngalo, katika maelezo yako ya polisi ilieleza una miaka 43 ni kweli au siku kweli.
Shahidi: Ni Kweli.
Wakili Ngalo: Ni kweli kuwa kwa mahesabu ulizaliwa mwaka 1966.
Shahidi: Ni Kweli.
Wakili Ngalo: Je ni kweli mwaka 1978 ulijiunga na JKT.
Shahidi: Ni kweli.
Wakili Ngalo: Kwa hiyo ulijiunga na JKT ukiwa na miaka 12.
Shahidi: Kwa mahesabu yako.
Wakili Ngalo: Darasa la saba ulianza mwaka gani
Shahidi: Mwaka 1970.
Wakili Ngalo: Ni nani aliyeshauri James Millya Kwenda polisi kumshitaki Sendeka
Shahidi: Ni Mkuu wa mkoa wa Singida Parceko Kone.
Wakili Mwaluko: Kwa hiyo, Shahidi ulijiunga na JKT ukiwa na miaka 12.
Shahidi: Kimya.
Wakili Mwaluko: Hebu tupige mahesabu chukua kalamu na karatasi chukua mwaka 1966 na utoe mwaka 1978.
Shahidi: Miaka 12.
Wakili Mwaluko: Je kuna jeshi ambalo linapokea watoto wa umri huo
Shahidi: Kimya.
Wakili Kamara: Je ni kweli kuwa wewe hukuona wakati Sendeka akimpiga kibao Millya.
Shahidi: Sikuona.
Wakili Kamara: Ni kweli pia wewe hukuona wala kusikia kilichotokea kabla ya Millya kuanguka chini.
Shahidi: Ni kweli.
WakiliKamara: Ni Kweli kuwa ulikuwa hujui tukio la kupigwa Millya hadi Millya mwenyewe alipokueleza.
Shahidi: Ni Kweli.
Wakili Kamara: Katika maelezo uliyotoa hapa umesema baada ya kumuona Sendeka na bastola ulisemaje.
Shahidi: Huwiii Sendeka anaua mkuu wa mkoa.
Wakili Kamara: Je katika maelezo yako ya polisi hebu tusomee uliandika hivyo.
Shahidi: Anasema niliandika Sendeka anaua.
Wakili Kamara: Je baada ya kuyapitia hayo maelezo ulisema yamekosewa.
Shahidi: hapana.
Wakili Kamara: Unasema ulipogeuka wakati wa chakula ulimuona Sendeka amemuelekezea bastola Millya je nani alikuwa mbele yako.
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili Kamara: Nani alikuwa nyuma yako
Shahidi: Mimi ni mgeni wilayani Monduli, siwakumbuki kwa majina ila ambaye alikwenda kumwondoa Sendeka alikuwa na mbunge wa Ngorongoro, Saningâo Ole Telele.
Katika kesi hiyo, Sendeka anatuhumiwa kumpiga kibao Millya ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha na kumtishia na bastola Januari 9 mwaka huu, Wilayani Monduli kitu ambacho ni kinyume sheria.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa shahidi wa tano kutoa ushahidi wake ambapo, upande wa mashitaka unawakilisha na wanasheria wa serikali Michael Luena na Hashim Ngole. http://www.facebook.com/sharer.php?u=http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15280