Duh CCM bwana eti aliingia JKT ana miaka 12

Mvutakamba

Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
58
Reaction score
1
Katibu UVCCM apata wakati mgumu kesi ya Sendeka

Na Mussa Juma, Arusha

KATIBU wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Wilaya ya Monduli, Mathias Mihayo (43) ambaye ni Shahidi wa nne katika kesi shambulio na kutishia kwa silaha inayomkabili Mbunge wa Simanjiro Christopha Ole Sendeka(CCM) jana alipata wakati mgumu mahakamani baada ya kudai alijiunga na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) akiwa na miaka 12.

Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, James Kalehemaha katika kesi hiyo inayohudhuriwa na mamia ya watu, Shahidi huyo alisema ana umri wa miaka 43 na alijiunga na JKT mwaka 1978.

Akihojiwa na mawakili wa utetezi, Mihayo alisema alizaliwa mwaka 1966 na alimaliza darasa la saba mwaka 1976 katika shule ya Msingi Solwa Mkoani Shinyanga na mwaka 1978 alijiunga na JKT kambi ya Makotopola mkoani Dodoma.

Sehemu ya mahojiano baina ya Mawakili wa Utetezi, James Ngaro, Hezra Mwaluko na Mpaya Kamara na Shahidi huyo yalikuwa ni hivi.

Wakili Ngalo, katika maelezo yako ya polisi ilieleza una miaka 43 ni kweli au siku kweli.

Shahidi: Ni Kweli.

Wakili Ngalo: Ni kweli kuwa kwa mahesabu ulizaliwa mwaka 1966.

Shahidi: Ni Kweli.
Wakili Ngalo: Je ni kweli mwaka 1978 ulijiunga na JKT.
Shahidi: Ni kweli.

Wakili Ngalo: Kwa hiyo ulijiunga na JKT ukiwa na miaka 12.
Shahidi: Kwa mahesabu yako.

Wakili Ngalo: Darasa la saba ulianza mwaka gani
Shahidi: Mwaka 1970.

Wakili Ngalo: Ni nani aliyeshauri James Millya Kwenda polisi kumshitaki Sendeka
Shahidi: Ni Mkuu wa mkoa wa Singida Parceko Kone.
Wakili Mwaluko: Kwa hiyo, Shahidi ulijiunga na JKT ukiwa na miaka 12.
Shahidi: Kimya.
Wakili Mwaluko: Hebu tupige mahesabu chukua kalamu na karatasi chukua mwaka 1966 na utoe mwaka 1978.

Shahidi: Miaka 12.
Wakili Mwaluko: Je kuna jeshi ambalo linapokea watoto wa umri huo
Shahidi: Kimya.
Wakili Kamara: Je ni kweli kuwa wewe hukuona wakati Sendeka akimpiga kibao Millya.
Shahidi: Sikuona.
Wakili Kamara: Ni kweli pia wewe hukuona wala kusikia kilichotokea kabla ya Millya kuanguka chini.
Shahidi: Ni kweli.

WakiliKamara: Ni Kweli kuwa ulikuwa hujui tukio la kupigwa Millya hadi Millya mwenyewe alipokueleza.
Shahidi: Ni Kweli.

Wakili Kamara: Katika maelezo uliyotoa hapa umesema baada ya kumuona Sendeka na bastola ulisemaje.

Shahidi: Huwiii Sendeka anaua mkuu wa mkoa.

Wakili Kamara: Je katika maelezo yako ya polisi hebu tusomee uliandika hivyo.
Shahidi: Anasema niliandika Sendeka anaua.
Wakili Kamara: Je baada ya kuyapitia hayo maelezo ulisema yamekosewa.
Shahidi: hapana.

Wakili Kamara: Unasema ulipogeuka wakati wa chakula ulimuona Sendeka amemuelekezea bastola Millya je nani alikuwa mbele yako.
Shahidi: Sikumbuki.

Wakili Kamara: Nani alikuwa nyuma yako

Shahidi: Mimi ni mgeni wilayani Monduli, siwakumbuki kwa majina ila ambaye alikwenda kumwondoa Sendeka alikuwa na mbunge wa Ngorongoro, Saning’o Ole Telele.

Katika kesi hiyo, Sendeka anatuhumiwa kumpiga kibao Millya ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha na kumtishia na bastola Januari 9 mwaka huu, Wilayani Monduli kitu ambacho ni kinyume sheria.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa shahidi wa tano kutoa ushahidi wake ambapo, upande wa mashitaka unawakilisha na wanasheria wa serikali Michael Luena na Hashim Ngole.
http://www.facebook.com/sharer.php?u=http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15280
 
du hii kali, kama JKT zamani walikuwa wanachukua watoto kujiunga na jeshi sioni sababu ya kulirudisha hilo jeshi, coz lina kandamiza haki za watoto
 
Cha kufurahisha ni kuwa kamaliza darasa la saba mwaka 1976 yaani akiwa na miaka 10 tu! Kweli huyu alikuwa Kipanga...
 
Cha kufurahisha ni kuwa kamaliza darasa la saba mwaka 1976 yaani akiwa na miaka 10 tu! Kweli huyu alikuwa Kipanga...

sio tu kipanga ila morphology yake nayo bab kubwa. Unajua zamani kipimo cha kuruhusu mtoto kuanza darasa la kwanza ni mkono wa kulia kufikia au kupita sikio la kushoto unapowekwa juu ya kichwa.Kabla ya miaka saba mazee huja qualify unless una bodi kubwa kiaina!
 
Cha kufurahisha ni kuwa kamaliza darasa la saba mwaka 1976 yaani akiwa na miaka 10 tu! Kweli huyu alikuwa Kipanga...

CCM ndivyo walivyo, nyie mnashangaa lakini kwa wao hawaoni ubaya wowote wala kichefuchefu hawana
 
Alizaliwa 1966 na kuanza msingi 1970 .... ile ya yule jamaa wa mwanza ni cha mtoto
 
Alizaliwa 1966 na kuanza msingi 1970 .... ile ya yule jamaa wa mwanza ni cha mtoto


CVs za viongozi CCM zinastahili kuwekwa Ze komedi.

Subiri uchaguzi uingie. mara hii nadhani woote watakuwa na Ph.Ds. zila za miezi 6.

Wengine wanaitwa vijana wakiwa na miaka 60
Wengine sasa hivi wako juu lakini hakuna dalili za mafanikio huko nyuma walikopitia.
 
Hii ndio shida ya ushahidi wa kupanga ambao waendesha mashitaka wa kibongo hujaribu kufanya ili wa win case.

Haya ndio matokeo. Mtu hajui miaka hata aliyokwenda shule wala JKT kwa nini mahakama imuamini mtu kama huyu?
 
Hii ndio shida ya ushahidi wa kupanga ambao waendesha mashitaka wa kibongo hujaribu kufanya ili wa win case.

Haya ndio matokeo. Mtu hajui miaka hata aliyokwenda shule wala JKT kwa nini mahakama imuamini mtu kama huyu?

Sidhani kama hajui miaka aliyoenda shule wala JKT, kilichotokea hapo na kinachotokea kwa sehemu kubwa ya jamii yetu ni kuwa wakati mtu amefika umri fulani anapunguza miaka yake ili apate nafasi ya kazi au uongozi. Siwezi kushangaa huyu alipunguza miaka yake hiyi ili abaki kwenye uongozi wa UVCCM
 

hahahahaha,

mambo mengine bwana, kwa hiyo jamaa kajipunguzia umri ili awe kiongozi wa vijana? Mbona Kikwete ana miaka karibu 60 lakini watu wanamwita eti ni kijana? Jamaa angepull ukikwete tu mambo yangekuwa poa.
 

Hata mimi nashangaa.
Watu design hii hii utasikia eti kachaguliwa kamanda wa vijana wa wilaya au mkoa!
Ni aibu tupu.
 
Hata mimi nashangaa.
Watu design hii hii utasikia eti kachaguliwa kamanda wa vijana wa wilaya au mkoa!
Ni aibu tupu.


Unaweza kukuta baada ya Uchaguzi anakuwa Mkuu wa Wilaya . Angalia wakuu wa wilaya tulio nao leo .
 
Kazaliwa 1966, kamaliza la saba 1976!! alianza darasa la kwanza lini? alisoma madarasa mangapi? Jeshi lipi hilo linatoa ajira kwa watoto?? huyo ndio kiongozi wa VIJANA???!!! Kachemsha..kaaazi kwelikweli!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…