Hehehe!! Kweli mumedhamiria kutumia nguvu nyingi, maana ndio mara ya kwanza kwangu mimi kuona ukiandika insha humu, nimezoea kuona ukiandika sentensi moja na kutoweka. Lakini jitahidi kuboresha uandishi wako, kiswahili chako kibovu sana.
Huu uchaguzi unaokaribia ndio sababu kuu za nyie kusuasua kwenye suala la corona, maana mlipozembea kuchukua hatua kabla corona haijatamalaki, upinzani waliwasema sana na kama mngeendelea kutangaza namba za waathirika zilizokua zinapanda, mngezama nyie MaCCM, maana ilikua kila mkitangaza idadi ya waathirika wapya, Mbowe alikua anaibuka na kuhutubia taifa.
Kwa kifupi hapo tayari wapinzani walikua wameanza kuteka mioyo ya Watanzania.
Sasa kwa hili la kuficha na kuaminisha Watanzania kwamba corona imeisha na wengi wao walivyo Wadanganyika wameishia kuamini, sasa inasababisha muwe na hasira sana mkisikia majirani wanawapima na kutaja mamia ya madereva wenu wanaogelea kwenye corona, na ndio maana mkaomba taarifa za waathirika wenu zifichwe, ila baada ya uchaguzi na CCM kuchukua uongozi tena hamtakua na lolote la kuogopa, mtataja moja kwa moja, ila kwa sasa mkiachia tu, wapinzani watatumia hiyo fursa ya kuibuka kidedea.