Duka la mafuta ya taa la Mama Maria Nyerere Kariakoo na Magomeni

Duka la mafuta ya taa la Mama Maria Nyerere Kariakoo na Magomeni

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
DUKA LA MAFUTA YA TAA LA MAMA MARIA NYERERE KARIAKOO NA MAGOMENI 1955

Duka la kwanza la Mama Maria Nyerere lilikuwa Mtaa wa Livingstone na Mchikichi kisha Mama Maria akafunga duka hili la Kariakoo kwa ajili ya umbali baada ya kuhamia Magomeni Maduka Sita kwa msaada wa Ali Msham aliyekuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu, Ali Msham akamfungulia Mama Maria duka nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu palipokuwa na tawi la TANU.

''Nikiwa mtoto nakumbuka sana vipi baba akishughulishwa na kutaka kuona kuwa Mama Maria na watoto wake hawakosi chochote kuyafanya maisha yao kuwa mepesi, ya starehe na furaha akihakikisha chakula kinapelekwa dukani kwa Mama Maria kila siku katika duka lake dogo lilikuwapo Mtaa wa Livingstone kona na Mtaa wa Mchikichi, hiki kikiwa kielelezo chake kikubwa kabisa cha huruma na ukarimu wake.''

Aisha ''Daisy'' Sykes (2018)

 
Mzee nitazidi kukushangaa cku hadi cku

Hujaeleza kiundani namna Mama Maria akiendesha biashara zake ikiwemo kutaja mafanikio & changamoto n.k
 
Mzee Mohamed

Bado hujabadilika tu!

Kichwa Cha habari na maelezo ya ndani havifanani kabisa

Naamini kabisa ulikusudia kutaja Waislamu wenzako Kwamba kuwa bila wao( Msham & Skyes) duka la Mama Maria lisingefunguliwa au kuendelezwa!
Takbiiiir Takbiiiir Takbiiiir
 
Tunafaham wakristo wengi walikuwa wananeemeka na ukoloni hence hawakujishugulisha saana na kupigania uhuru, waislam wengi pia walikuwa wananyanyasika sana na ukoloni hence walijitoa saana kupigania uhuru.

Lastly, tunafaham kuwa Mwalim aliwaweka bench waislam baada ya kupata uhuru ingawa wao ndo waliomsaidia zaidi katika juhudi za kupata uhuru

Lastly, inafahamika kuwa historia ya waislam wengi imefichwa ndo maana elim yetu ya historia imejaa zaidi issue za ukolon kuliko kujivunia juhudi za kupigana na ukoloni
 
Mzee wangu naomba uwe unanitag ukiwa unaanzisha thread.

Asanta.
 
Tunafaham wakristo wengi walikuwa wananeemeka na ukoloni hence hawakujishugulisha saana na kupigania uhuru, waislam wengi pia walikuwa wananyanyasika sana na ukoloni hence walijitoa saana kupigania uhuru.

Lastly, tunafaham kuwa Mwalim aliwaweka bench waislam baada ya kupata uhuru ingawa wao ndo waliomsaidia zaidi katika juhudi za kupata uhuru

Lastly, inafahamika kuwa historia ya waislam wengi imefichwa ndo maana elim yetu ya historia imejaa zaidi issue za ukolon kuliko kujivunia juhudi za kupigana na ukoloni
Ila Nyerere alikua fundi Sana aisee,alikaribishwa mjini na akapindua meza kibabe.
 
Mzee Mohamed

Bado hujabadilika tu!

Kichwa Cha habari na maelezo ya ndani havifanani kabisa

Naamini kabisa ulikusudia kutaja Waislamu wenzako Kwamba kuwa bila wao( Msham & Skyes) duka la Mama Maria lisingefunguliwa au kuendelezwa!
Uzalendo...
Nifafanulie kuhusu hili la mabadiliko.

Ama hili la nafasi ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika ndiyo historia ilivyokuwa.

Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake na akampa Mama Maria Nyerere sehemu katika nyumba yake aweke duka.

Mimi najifaharisha sana na historia hii.

Ikiwa wewe unakuudhi hii ni bahati mbaya kwako.
 
Wa kupuliza,
Historia ya TANU sasa inafahamika na nimeiandika Mwalimu Nyerere akiwa hai na kaisoma.

Si kweli kuwa historia hii ilibakia chembelecho, "imepinduliwa."

Soma hapo chini moja ya vile ambavyo Mwalimu alisoma:

"Baada ya kuundwa kwa TANU Nyerere akiwa Rais wake ikaamuliwa kuwa aende kukisajili chama kwa Msajili.

Abdul, Ally Sykes na Nyerere wakakubaliana kuwa Nyerere akishakamilisha usajili wakutane nyumbani kwa Ally Mtaa wa Kipata.

Kisa hiki amenihadithia Bi. Zainab mbele ya mumewe Ally Sykes.

Bi. Zainab anasema Nyerere alipofika Kipata moja kwa moja akajitupa kwenye sofa hoi kachoka taaban.

Jua lilikuwa kali nje.

Uso wa Nyerere ulionesha kuwa mambo hayakwenda vizuri kwa Msajili.

Wote watatu wakawa wametulia wanangoja kumsikiliza Nyerere awake taarifa.

Msajili amekataa kuisajili TANU kwa kuwa Nyerere alikuwa hana rejesta buku la kuonyesha wanachama wa TANU.

Hapo hapo Abdul Sykes akatoa oda akasema niititieni Mzee Said Chamwenyewe.

Mzee Said Chamwenyewe akapewa kadi za TANU na rejesta buku Abdul akamwambia, "Mzee Chamwenyewe nenda Rufiji katuletee wanachama."

Hivi ndivyo ikawa kundi kubwa la wanachama wa mwanzo wa TANU walitoka Rufiji.

Rufiji ilikuwa moja ya himaya za Mufti Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa pia ni Khalifa wa Quadiriyya.

Hapakuwa na shida ya kuwapata wanachama kwani bila shaka taarifa za TANU kutoka kwa Khalifa zimeshatangulia.

Kadhalika mbele ya Rufiji kuelekea Kilwa Shadhuly chini ya Sheikh Nurdin Hussein ilikuwa na wafuasi wengi na Sheikh Nurdin mwenyewe alikuwa karibu sana na Sheikh Hassan bin Ameir.

Kote huku TANU ilizoa wanachama.

Lakini nguvu hii maadui wa TANU iliwatia hofu wakaanza kueneza propaganda kuwa Waislam wanatayarisha Maji Maji nyingine dhidi ya Waingereza.

Waingereza walimzungusha sana Nyerere katika kutoa tasjila lakini ilipofika tarehe 30 November, 1954 Msajili alimkabidhi Mwalimu tasjila ya TANU.

Ally Sykes akachapisha kadi 1000 za kwanza za TANU kutoka mfukoni kwake kisha akachapisha kadi 2000 kutoka fedha alizokopa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) yeye akiwa Secretary.

Kadi No. 1 alimwandikia Julius Kambarage Nyerere, TANU Territorial President, kadi no. 2 akajiandikia mwenyewe, kadi no. 3 akamwandikia kaka yake Abdulwahid, kadi no 4 Dossa Aziz, kadi no. 5 Dennis Phombeah kabila Mnyasa kutoka Nyasaland, kadi na 6 Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya na kadi no 7 Abbas Sykes."

Wewe umesoma hayo hapo juu na kama ulikuwa hujui sasa unajua.

Mimi nakuandikia kwa adabu na heshima kwako na kwa Mwalimu Nyerere.

Jiepushe na hizi lugha za kejeli za "kupindua," nk. kwani unamfedhehesha Nyerere.

Mimi nimeishi katika historia hii lau nilikuwa mtoto mdogo.

Wazee wangu hao unaowasoma katika maandishi yangu wanastahili heshima.
 
Back
Top Bottom