Duka la nguo (Fashion), Tsh 15 milioni zinatosha?

Duka la nguo (Fashion), Tsh 15 milioni zinatosha?

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2011
Posts
303
Reaction score
154
Nina mpango wa kumfungulia mke wangu biashara. Mimi ni mtumishi na kwa kipato changu naweza kukopa benki mpaka Tsh 15 milioni. Je, zinatosha kwa duka la nguo za wanawake na watoto? Duka hilo nataka kuliweka mkoani kigoma ambapo frem ya duka ni kiasi cha Tsh 150,000 kwa mwezi.

Je, kwa Dar ninaweza kupata wapi mzigo wa jumla wenye nguo nzuri na za kisasa?

Wenye uzoefu na masuala haya ya Fashion naombeni ushauri wenu.
 
Mkuu Mbavu za Mbwa Hizo ni pesa ya kutosha kabisa. Sijajua upo mji gani... Mtaji mara nyingi wote hutosha tegemeana na mahala ulipo na ni biashara ya level ipi unataka kufanya.

Biashara ya nguo za wanawake na watoto zimepisha level.. Kuna maduka ambayo huuza nguo za kawaida (kama vile ma dera ya wanawake na mitandio), kuna maduka ambayo huuza nguo za mitoko na maofisini, na kuna wale wenye nguo za bibi harusi na wasimamizi wake (Hii sidhani kama ndiyo wataka thou).

Ukija suala la chumba nalo ni kitu cha kuzingatia... Mahala/Ukubwa na hadhi ya chumba tokana na wateja uliyolenga. Kuchagua ni aina zipi za nguo mkeo atajikita ni suala ambalo la kuzingatia sababu inapendeza sana mfanya biashara kuelewa bidhaa yake ili kuweza kutambua na kubashiri mzigo upi unafaa katika biashara. Ina maana utanunua mzigo tokana na eneo ulilopo la biashara.. Mfano huwezi fungua duka la nguo za harusi Masense ukauza vizuri kama vile ambavyo utafungua duka la dera ama kawaida.

Ni vema sana kutochukua kwanza mkopo huo hadi pale utakapo kua umekamilisha kutambua kila kitu kuhusu biashara yako. Kwa milioni 15 kuna wale wanaosafiri kwenda nje na kuna wale wanao ona ni kheri ifike walau Million 25--> kusafiri kwenda nje. The Best place utapata kununua jumla ni Kariakoo... Yapaswa tu kufanya savei, na kutembelea maduka kuuliza bei na taratibu zake ili kuweza kupata picha ya mzigo unaotakiwa.
 
Back
Top Bottom