Dully Sykes amtetea Harmonize kumuiga Diamond

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii Dully Sykes ametoa maoni yake baada ya tetesi za Harmonize kumuiga Diamond, mara baada ya watu kuzidi kutoa maoni yao baada ya kuachia video yake aliyomshirikisha.


Akizungumza kwenye Friday Night Live ya EATV, Dully Sykes alianza kwa kutetea kuwa hawafanani lakini baadae akaja kubadilisha upepo,na kusema Harmonize ana kila sababu ya kufanana na Diamond, kwani wasanii hao ni kama ndugu, hivyo sio kitu kibaya wakifanana kwenye baadhi ya mambo.

“Wana tofauti kwa sababu huyu hajazaliwa na koo la Diamond, kitu wanachomfanya wamfananishe na Diamond, hata mimi ukikaa na mtu sana utafanana nae kwa namna moja au nyingine, huyu Diamond ni kaka yake, anaishi na diamond anakaa na diamond, muache afanane nae”, alisikika Dully Sykes akimtetea Harmonize.

Hivi karibuni msanii huyo ameshushiwa tuhuma za kufanana au kuiga kama mashabiki walivyodai, kutoka kwa msanii Diamond Plutnumz, kuanzia anavyoimba mpaka mitindo ya kucheza.

Kwa upande wake Harmonize amekanusha kumuiga Diamond, kwani yeye hawezi kuwa kama Diomond.

 
Binafsi namwelewa sana Harmonize... simuungi mkono but I know it's a matter of time tu atabadilika! Binafsi, kitambo sana nilishafanya attempt kwenye game sema baadae nikaachana na hizo mambo! The problem ni kwamba nilikuwa nam-feel sana Sugu, tena sana! Sasa issue ikawa nikianza kutembea na mistari... ni Mr. II kwa 800% cuz' nilianza kutembea na mistari yake nikiwa Form I hadi nikiwa grown up boy!! Ilikuwa ni kazi ngumu kweli kweli mimi kuwa mimi though baadae nilibadilika! Na wala msidhani huyo Harmonize anapenda kutembea kama Chibu lakini ndo hivyo tena...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…