Dully Sykes: Sioi leo wala kesho, hata baba yangu hakuwahi kuoa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Baada ya kupost picha akiwa na Mwana FA baada ya kuoa na kuandika maneno yanayoashiria naye hivi karibuni atafuata nyayo za Mwana Fa, Dully Sykes ameruka viunzi na kusema hana mpango wa kuvuta jiko leo wala kesho.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully amesema yeye kwake kuoa ni sawa na maji kufuata mkondo, kwana hata marehemu baba yake hakuwahi kuoa wakati wa uhai wake.

“Kila mtu ana mipango yake, maji hufuata mkondo, wewe nafikiri mzazi wako alioa, mi baba yangu hakuwahi kuoa”, alisikika Dully akielezea sababu ya yeye kutoamua kuoa mpaka leo.

Pamoja na hayo Dully amesema akiona kuna umuhimu na ikiwezekana ataoa, hivyo amewataka wadau wake wamuombee ili aweze kuwa na mawazo ya kuoa na kuwa na mke rasmi.

“Kama inawezekana naweza kuvuta jiko, na kama haitowezekana sitavuta jiko, kwa sababu sijafikiria bado, mniombee nipate mawazo ya kuchukua jiko, sio kwa vile FA amefanya basi ndo uone inawezekana, nina sababu zangu tu mwenyewe, nikikwambia ntakuvunja moyo kama umeoa wewe”, alisema Dully Sykes.
 
ila ni kweli, kuna watu wengine mitindo yao ya maisha haiwaruhusu kufanya baadhi ya mambo, yani ndio dully
 
Alijenga heshima na jina zamani sasa bado anataka ujana tu?
 
ila ni kweli, kuna watu wengine mitindo yao ya maisha haiwaruhusu kufanya baadhi ya mambo, yani ndio dully
Nakuunga mkono. Lifestyle ya Dully ni ngumu. Ana watoto wanne. Kila mmoja na mama yake. Atakaemuoa atakubali mzigo huo plus wa kwake atakaowazaa?
 
issue ni kupata anayekufaa mjomba! ukiona mambo hayaendi vizuri unajipa moyo sijaamua hahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…