Steph Curry
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 5,936
- 4,707
Habarini wanajukwaa,
Mambo ni mengi muda mchache, poleni na mihangaiko ya kutia nia, mapigo ya wajumbe na sasa kusubiria mchakato wa mwisho wa kutangazwa na kampeni kuanza.
Kwa miaka hii mitano ya Mh. Magufuli wakulima wa Korosho wamekutana na kitu kinaitwa "mixed feelings" Yani hawaelewi kama wanapanda ama wanashuka, wanajikuta wapo wapo tu. Mh. Rais alisaidia sana zao la Korosho lianze kuchukuliwa serious kwanza na wakulima wenyewe waliopo mikoa ya kusini lakini pia macho wa waona fursa mbalimbali sehemu mbalimbali za nchi yetu. Mapori yalifyekwa, mashamba za zamani yaliotelekezwa yalifufuliwa, miche ilizalishwa na kusambazwa mikoa mbalimbali ya nchi yetu hii ni kwasababu tu KOROSHO ilionekana kama fursa ya kuaminika. Bei ilipanda kutoka wastani wa 1800 mpaka ikafika 3900-4000. Kona Kona nyingi na figisu kwenye zao hili zilimalizwa na zote hizi ni juhudi za Rais Magufuli. Na kusema tu ukweli, Kusini kulifunguka na kulianza kupendeza..
Msimu wa 2018/2019 sote tunajua kilichotokea, lakini Mimi pia kwa uzoefu wangu kwenye hii game ya Korosho niliandika thread humu kumtahadharisha Rais kwa hicho alichoamua kukifanya. Korosho sio Mkulima pekee, mpaka Korosho inapanda meli kwenda ng'ambo kuna mkono wa wadau wengi sana hapo katikati. Na wadau hao hutumia fedha zao au hata dhamana zao kwenye mabenki ili tu wapate mitaji ya kuhudumia Biashara hii ya Korosho. Mwaka ule ukiacha wakulima kutolipwa fedha zao, lakini wadau wengi pia waliumizwa.
Kuna wasafirishaji, kuna waendesha maghala, kuna wapuliziaji maghala, kuna mafundi wa mizani, kuna taasisi mbalimbali zinazotoa mikopo, kuna suppliers wengine wengi kwenye kuanzia Union (vyama vikuu) mpaka AMCOS. Hao wote hawakupewa hata senti, wengine walishauziwa dhamana zao, wengine walishajifia kwa msongo wa mawazo. Na kwa kumbukumbu hilo deni la 2018 ndio juzi Waziri Mkuu alitoa Billion 20 zilipe wakulima waliobakia pamoja na wadau wengine baada ya madeni yao kuhakikiwa kwa miaka miwili. Tunajua hayo hayakuwa mapendekezo ya Mh. Rais ila aliingizwa chaka tu na wajanja wajanja walewale wanaotegemea kuneemesha familia zao kwa mgongo wa zao hili.
Sasa mwaka huu serikali imekuja na kitu kinaitwa TMX, hatujui kama ni mkakati rasmi wa Serikali hii ya Mh. Magufuli au ni mkakati wa wajanja wachache pale Wizara ya Kilimo akiwemo huyu anayeitwa Bashe. Hawa TMX walianza majaribio kwenye zao dogo la Ufuta huko Mtwara. Uzalishaji wa Ufuta ni takribani Tani elfu 10 tu kwa mkoa wa Mtwara. Na hao TMX walikuwa na majukuma ya kuendesha mnada online, kulipa wakulima, kulipa wasafirishaji na kuwalipa AMCOS fedha zao za Ushuru (ambazo hizo ni fedha kwa ajili ya uendeshaji wa vyama vyao).
Lakini mpaka sasa ni kilio tu huko Mtwara, wakulima hawajalipwa, wasafirishaji wamelipwa nusu tu ya fedha zao, AMCOS hawajapewa Ushuru wao wote na malalamiko ni mengi kuliko kawaida. Pamoja na kwamba hao TMX wameperform vibaya na hakuna kokote wanakowajibishwa, na wakulima hawawataki kabisa lakini chini kwa chini tumesikia watu hawahawa ambao mpaka leo wameshindwa kuwalipa wakulima wa zao la Ufuta wanataka kujiingiza kwenye Korosho.
Korosho kwa mkoa wa Mtwara uzalishaji wake Ni takribani Tani 175,000 mpaka Tani 200,000 msimu Ukiwa mzuri. Sasa kama Tani elfu 10 za ufuta zimewashinda na walisema watalipa mkulima ndani ya siku 3 tu lakini cha kushangaza Kuna wakulima walipeleka ufuta wao tangia mwezi June ila mpaka sasa hawajalipwa wataweza kweli kulipa Tani laki mbili za Korosho?
Hili suala hatujajua kama Mh. Rais analijua, ila kama analijua na ameliridhia basi ajiandae tu akija kwenye kampeni kukutana na wakulima wake wanyonge wakiikataa hii TMX au hata wengine kudiriki kusema hawatapeleka mazao yao ghalani kuuza au ikibidi hata kwenda kuuzia Msumbiji. Wakulima wa Korosho pamoja na wadau hawataki kabisa adha ya 2018 ijirudie tena mwaka huu. Hao TMX wabaki kufanya minada huko kwenye choroko za Tani 40 ila kwenye zao kubwa kama Korosho kuwaruhusu hao watu ni kuendelea kuwaonea, kuwakandamiza na kuwaibia wakulima wa zao hili.
Bashe na wahuni wenzako uliowaweka pale LAPF Tower ambao pia tunazo taarifa pesa waliyoiba kwenye Ufuta umeanza kuwa tamu hivyo kutamani kuja kuiba mabilioni mengine kwenye Korosho, tunawakataa na tutawapinga. Wakati wakulima wa Korosho wanapata taabu kuna watu wanahangaika nao, wakati AMCOS zikiwa na matatizo na changamoto kuna wadau tunarekebisha, nyie mmekaa hapo LAPF hakuna mnachokifanya kazi mnayoitaka na kukamata pesa za wanyonge. Hii sio sawa kabisa.
Na tunasikia mmeshahonga kwa viongozi wa Mkoa wa Mtwara wawawekee kifua, eti mmetumwa na wakubwa, waambieni hao wakubwa waje huku shambani kulima na sio kutoa maagizo wakiwa Posta au Dodoma huku shida za mkulima hawazijui.
Tutashangaa sana kama TMX itaruhusiwa kuja kuhujumu zao la Korosho tena.