Duncan Edward alisema anarudi kesho yake, Lakini akarudishwa maiti

Duncan Edward alisema anarudi kesho yake, Lakini akarudishwa maiti

Mdakuzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,294
Reaction score
6,872
Jumanne, Januari 14, 1958
United iliichapa Red Star Belgrade mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Ulaya kwenye uwanja wa Old Trafford.

Jumatatu, Februari 3, 1958
Kikosi cha Manchester United kilikwea ndege ya kukodi kutoka Manchester kwenda Belgrade, Yugoslavia. Safari hiyo ilipangwa kupitia Munich kwa safari zote kwa ajili ya kujaza mafuta, baada ya ndege hiyo kukosa ruti ya moja kwa moja.

Saa chache baadaye wakiwa angani, wakakumbana na hali ya hewa mbaya, mawingu mazito, kushindwa kuona na barafu. Hali iko chini ya kiwango kinachoruhusiwa na shirika la British European Airways (waliowakodisha ndege hiyo) kuruhusu marubani kutua.

Hali inazidi kuwa mbaya kiasi kwamba mhandisi wa uwanja wa ndege wa Munich alishtukia tu ndege imetua wakati alipoiona ikiegeshwa.

Jumatano, Februari 5, 1958
United ilitoka sare ya mabao 3-3 naushindi wa mabao 4-0 wa Red Star Belgrade na kufanikiwa kusonga mbele kwenye nusu fainali ya Kombe la Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo.

Baada ya mechi, pati ya nguvu ikaandaliwa kwa ajili ya wachezaji ambayo ilifanyika kwenye Ubalozi wa Uingereza.

Alhamisi, Februari 6, 1958
Msafara huo, pamoja na abiria wengine watano walioongezeka - akiwemo mke na binti wa ofisa wa jeshi la anga katika Ubalozi wa Yugoslavia jijini London – uliondoka jijini Belgrade
wakati wa mawio kuelekea Manchester.

Safari ilichelewa kwa saa moja baada ya winga Johnny Berry kupoteza paspoti yake. Baadaye, ndege hiyo ikaondoka na kutua Munich kwa ajili ya kujaza mafuta, ambapo uwanja wa ndege umezingirwa na mawingu, mvua na barafu.

Kutua kwenye uwanja huo wa Munich kulimlazimu rubani, Kapteni James Thain, kutumia vifaa maalum vya kukabiliana na barafu, kwenye mabawa.

Baada ya kutua, msafara wa Manchester ulitoka kwenye ndege na kuingia kwenye jengo la uwanja huo, huku baadhi ya wachezaji wakitaniana na wafanyakazi waliokuwa wakijaza mafuta kwenye ndege.

Baada ya kukamilisha taratibu za kuondoka, abiria wote walirejea kwenye ndege, huku wafanyakazi wa ndege hiyo wakiikagua hasa kwenye mabawa.

Kwa tahadhari, mafuta ya kuzuia barafu yangeweza kupakwa kwenye mabawa ama barafu kutolewa, lakini wakaamua kuacha kutokana na mazingira yalivyokuwa.

Majira ya saa 8.20 mchana (GMT), takriban zaidi ya saa baada ya kuwasili, ndege hiyo ikawa tayari kwa kupaa. Hata hivyo, sauti isiyo ya kawaida kutoka kwenye injini ikamshtua rubani Kapteni Thain na msaidizi wake, Kapteni Kenneth Rayment.

Inaendelea...

Ova
 
Hata hivyo, sauti isiyo ya kawaida kutoka kwenye injini ikamshtua rubani Kapteni Thain na msaidizi wake, Kapteni Kenneth Rayment, na kuwafanya waahirishe kuruka.

Wawili hao wakaamua kujaribu tena, lakini jaribio hilo la pili likaahirishwa tena kwa sababu zile zile, likielezwa na Kapteni Thain kwa abiria wake kama "tatizo dogo la injini" ambalo lingewalazimu kurudi mahali pa kuegesha na kuikagua injini.

Kila mtu akashuka kwenye ndege tena, na wakati wakielekea sehemu ya kuondokea, mchezaji nyota wa Man United Duncan Edwards akatuma telegram kwa mama mwenye nyumba wake ikisema - "Ndege zote zimeahirishwa. Tutarudi nyumbani kesho. Duncan." Bila kutegemea, abiria wote wakaitwa tena kurudi kwenye ndege.

Mnamo saa 9.04 alasiri, jaribio la tatu la kuruka linafanyika. Ndege inashindwa kupata kasi ya kupaa juu na kuanguka kwenye uzio wa uwanja wa ndege na kisha kwenye nyumba ya jirani.

Bawa la injini na sehemu ya mkia vikavunjika na ndege ikalipuka. Mti ukaangukia sehemu ya mbele, wakati sehemu ya katikati ikagonga kibanda, na ufanya lori lililokuwa limebeba magurudumu pamoja na mafuta likiwa limeegeshwa pembeni likalipuka.

Inaendelea...

Ova
 
Wakati huduma za dharura zinafika eneo la tukio, watu 21 walikuwa wamekufa - wakiwemo wachezaji saba, waandishi nane, wakala wa kampuni ya usafiri aliyeandaa safari hiyo na shabiki mmoja aliyeongozana na timu.

Baada ya saa mbili, utafutaji wa manusura ukaahirishwa, lakini alikuwa mwandishi wa habari wa Kijerumani aliyempata Kenny Morgans akiwa amebanwa kwenye mabaki ya ndege yapata saa tano tangu kutokea kwa ndege hiyo.

Manusura wakapelekwa kwenye Hospitali wa Rechts der Isar jijini Munich.

Miongoni mwao ni Albert Scanlon, ambaye alikaa bila kujitambua kwa wiki tatu, mshambuliaji nyota Bobby Charlton, ambaye alipata majeraha kidogo kichwani, na Johnny Berry na Jackie Blanchflower, ambao majeraha yao yalimaanisha hawatacheza tena.

Kocha Matt Busby alivunjika mbavu, pafu lilipasuka na majeraha mguuni. Hali yake ilikuwa mbaya kiasi kwamba alipewa uangalizi maalum na taarifa ya hospitali ilieleza kwa kifupi "hatuna matumaini ya kumuokoa".

Ijumaa, Februari 7, 1958
Miili ya marehemu ilisafirishwa kupelekwa Uingereza na kulazwa usiku kucha kwenye chumba cha mazoezi kwenye Uwanja wa Old Trafford kabla ya kuchukuliwa na ndugu zao kwa maziko.

Maelfu ya watu walijitokeza mitaani kwa ajili ya maziko, huduma za kumbukumbu zikafanyika kila mahali nchi nzima na ukimya wa dakika mbili ulitawala kabla mechi zote kuchezwa.
Kulikuwa na uvumi kwamba klabu hiyo ingekufa kwani wangeshindwa kumalizia michezo yake iliyosalia msimu huo au kushindwa kujenga timu tena.

Inaendelea...

Ova
 
Jumatano, Februari 19, 1958
Kulikuwa na taarifa kwamba Matt Busby alikuwa amepatiwa tiba za hali ya juu kwa mara ya pili, wakati Duncan Edwards na rubani msaidizi Kenneth Rayment hali zao ziliendelea kuwa mbaya siku hadi siku.

Pamoja na hayo, kikosi cha kuungaunga cha wachezaji 11 wa Man United kilikabiliana na Sheffield Wednesday katika raundi ya tano ya Kombe la FA.

Jalada la mbele la program ya mechi hiyo lilisomeka "United will go on (United itaendelea)" na hata kwenye karatasi ya orodha ya timu kulikuwa na maandishi, "kuna nafasi 11 wazi za kuzibwa".

Busby alimpigia simu msaidizi wake Jimmy Murphy akiwa kitandani hospitali akimweleza "endelea kupeperusha bendera". United ikashinda 3-0.

Ijumaa, Februari 21, 1958
Duncan Edwards alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata. Wiki moja baadaye Ken Rayment naye akafariki na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 23.

Matt Busby alipata nafuu kidogo wakati hali yake ikiendelea vyema, akasafirishwa kwenye Interlaken nchini Uswisi kuungana na mkewe, Jean.

Jumamosi, Machi 8, 1958
Ujumbe kutoka kwa kocha Busby ulichezwa wakati wa kuelekea kwenye mechi ya United. Gazeti la The News of the World likaripoti "wanawake walilia wakati rekodi ya sauti ya Matt Busby iliposikika kwenye uwanja uliojaa ukimya wa Old Trafford".

Ijumaa, Aprili 18, 1958
Matt Busby akarejea Manchester kwa mara ya kwanza, siku 71 baada ya ajali. Alisafiri kwa treni na meli kutoka Uswisi.

Inaendelea...

Ova
 
Jumamosi, Mei 3, 1958
Pamoja na mkanganyiko wa msimu huo, chini ya uongozi wa Jimmy Murphy, United ilifuzu kwa fainali ya Kombe la FA, ambapo siku hiyo walikuwa wanacheza na Bolton Wanderers.

Ni Murphy aliyeiongoza timu iyo, wakati Matt Busby alijikongoja na kuketi kwenye benchi akitumia mkongojo. Timu hiyo ilivaa jezi ambazo zilikuwa na picha ya phoenix akitokea kwenye miali ya moto.

Pamoja na jitihada hizo, mechi hiyo ilikuwa ngumu kwa timu iliyokuwa inachechemea ambapo Man United ilichapwa mabao 2-0.

Alhamisi, Mei 8, 1958
United iliifunga AC Milan mabao 2-1 katika mechi ya nyumbani ya nusu fainali ya Kombe la Ulaya.

Jumatano, Mei 14, 1958
AC Milan iliifunga United 4-0 kwenye Uwanja wa San Siro na kuitoa kwenye Kombe la Ulaya.

UEFA ilitoa ofa kwa Chama cha Soka cha England (FA) kuingiza United kwenye mashindano ya Kombe la Ulaya msimu unaofuata kama fadhila kwa kupoteza wachezaji na maofisa wake kwenye ajali ya ndege.

FA ilikataa, ikaamua kuipeleka Wolverhampton Wanderers, ambayo ndiyo ilikuwa bingwa wa ligi.

Ova
 
Umetuletea story ya klabu yako pendwa Ulaya, asante mchumba.

Ningependa kufahamu mwenye nyumba aliyetumiwa ujumbe na mchezaji aliyekuwa mpangaji wake alizipokea vipi taarifa hizo za ajali.
 
Umetuletea story ya klabu yako pendwa Ulaya, asante mchumba.

Ningependa kufahamu mwenye nyumba aliyetumiwa ujumbe na mchezaji aliyekuwa mpangaji wake alizipokea vipi taarifa hizo za ajali.
Sawa mrembo, nitazileta.

Ova
 
Story nzuri na ya kusisimua, kila niki waza watu wanavyo fariki wakiwa wadogo.

naishia kujipa moyo life must go on
 
Jumamosi, Mei 3, 1958
Pamoja na mkanganyiko wa msimu huo, chini ya uongozi wa Jimmy Murphy, United ilifuzu kwa fainali ya Kombe la FA, ambapo siku hiyo walikuwa wanacheza na Bolton Wanderers.

Ni Murphy aliyeiongoza timu iyo, wakati Matt Busby alijikongoja na kuketi kwenye benchi akitumia mkongojo. Timu hiyo ilivaa jezi ambazo zilikuwa na picha ya phoenix akitokea kwenye miali ya moto.

Pamoja na jitihada hizo, mechi hiyo ilikuwa ngumu kwa timu iliyokuwa inachechemea ambapo Man United ilichapwa mabao 2-0.

Alhamisi, Mei 8, 1958
United iliifunga AC Milan mabao 2-1 katika mechi ya nyumbani ya nusu fainali ya Kombe la Ulaya.

Jumatano, Mei 14, 1958
AC Milan iliifunga United 4-0 kwenye Uwanja wa San Siro na kuitoa kwenye Kombe la Ulaya.

UEFA ilitoa ofa kwa Chama cha Soka cha England (FA) kuingiza United kwenye mashindano ya Kombe la Ulaya msimu unaofuata kama fadhila kwa kupoteza wachezaji na maofisa wake kwenye ajali ya ndege.

FA ilikataa, ikaamua kuipeleka Wolverhampton Wanderers, ambayo ndiyo ilikuwa bingwa wa ligi.

Ova

UEFA ilitoa ofa kwa Chama cha Soka cha England (FA) kuingiza United kwenye mashindano ya Kombe la Ulaya msimu unaofuata kama fadhila kwa kupoteza wachezaji na maofisa wake kwenye ajali ya ndege.

FA ilikataa, ikaamua kuipeleka Wolverhampton Wanderers, ambayo ndiyo ilikuwa bingwa wa ligi.

Kwa nini?
 
Kwa sababu kuwapoteza waliokufa kwenye Ajali ile wakitumikia michuano ya Ulaya hakuwezi kufidiwa kwa fadhila ya kushiriki michuano bila jasho.

Ova
 
Back
Top Bottom